Thursday, January 30, 2014

SIDO Singida yawataka wajasiriamali kutumia mikopo kuimarisha ndoa zao.

Meneja wa SIDO mkoa wa Singida, Shoma Kibende akitoa nasaha zake muda mfupi kabla hajatoa mikopo yenye thamani ya shilingi 18.9 kwa wajasiriamali wa kikundi cha Urafiki cha mjini Singida.Kulia (aliyekaa) ni katibu wa kikundi cha urafiki,Remiji Alex.
 Meneja wa SIDO mkoa wa Singida,Shoma Kibenda,akimkabidhi Remji Alex mkopo wa shilingi 500,000.
Meneja mikopo wa SIDO mkoa wa Singida, Ruben Mwanja akitoa mafunzo kwa wajasiriamali muda mfupi kabla ya kukabidhi mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi 18.9 milioni kwa kikundi cha urafiki cha mjini Singida.
Meneja mikopo wa SIDO mkoa wa Singida, Ruben Mwanja (wa kwanza kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wanakikundi cha wajasiriamali cha Urafiki cha mjini Singida.Kikundi hicho kilikopeshwa zaidi ya shilingi 18.9 milioni na watarudisha na fidia ya shilingi 1.8 kwa mwezi.

MENEJA mikopo wa shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) mkoa wa Singida,Ruben Mwanja,amewataka wajasiriamali kutumia mikopo yao vizuri na kwa malengo yaliyokusudiwa,na pia mikopo hiyo isaidie kuimarisha ndoa zao.

Mwanja aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi mikopo mbalimbali yenye thamani ya shilingi 18,9 milioni kwa wanachama 39 wa kikundi cha Urafiki cha Singida mjini.

Amesema uzoefu unaonyesha wazi kwamba baadhi ya wanawake wanaobahatika kupata mikopo,hukorofishanana au kutengana kabisa wanaume wao.

“Pia wapo baadhi ya wanaume wakishapata mkopo wa kuendeleza biashara yao,hukimbilia kuoa mke mwingine”,amesema Mwanja na kuongeza;

“Nawasihi sana,mikopo ya SIDO isitumike kuongeza wake wengine au kuvunja ndoa za watu,itumike tu kuendeleza biashara ya mkopaji ili kupanua/kuongeza kipato cha mhusika”.

Kwa upande wake meneja wa SIDO mkoa wa Singida,Shoma Kibenda,alikipongeza kikundi cha Urafiki kwa madai kwamba kina utamaduni mzuri wa kurudisha mikopo kwa wakati na bila matatizo.

Kibenda aliwataka wapige hatua zaidi kwa kuangalia uwezekano wa kuanzisha viwanda vidogo kama njia moja wapo ya kujiongezea kipato zaidi.


Mikopo iliyotolewa juzi,kima cha chini kilikuwa shilingi

Nyalandu apongezwa na wapiga kura wake.

Waziri Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu akisalimiana na mwenyekiti mstaafu wa CCM wilaya ya Singida, Swalehe Msuri katika viwanja vya Mtinko jimbo la Singida Kaskazini.Waziri Nyalandu alikuwa Mtinko kuhudhuria hafla ya kupongewa kuwa waziri kamili wa Maliasili na Utalii.
Waziri Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhiwa mkuki na mzee Ntandu ili akautumie katika kupambana na ujangili.Nyalandu alikabidhiwa mkuki huo kwenye hafla ya kumpongeza iliyofanyika katika kijiji cha Mtinko kwa kuteuliwa kuwa Waziri Maliasili na Utalli.
Waziri Maliasli na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu akizungumza kwenye hafla ya kupongezwa na wapiga kuwa wake wa jimbo la Singida Kaskazini kwa kuteuliwa kuwa waziri kamili wa Wizara hiyo ya Maliasili na Utalii.Hafla hiyo iliyofana,ilifanyikia kwenye viwanja vya ofisi ya kijiji cha Mtinko.
Baadhi ya viongozi wilaya ya Singida waliohudhuria halfa ya kumpongeza Mh. Lazaro Nyalandu kwa kuteuliwa kuwa Waziri Maliasli na Utalli.Hafla hiyo iliyofana ilifanyikia katika kijiji cha Mtinko jimbo la Singida kaskazini.
Baadhi ya wananchi wa jimbo la Singida kaskazini waliohudhuria hafla ya Waziri Maliasili na Utalii, Mh.Lazaro Nyalandu kwa kuteuliwa kuongoza wizara hiyo.

SIDO yatoa mikopo ya zaidi ya shilingi 966 milioni kwa wafanyabiashara.

Meneja wa mikopo wa SIDO mkoa wa Singida, Ruben Mwanja akiwa ofisini kwake akiwajibika katika majukumu yake ya kila siku.
Jengo la ofisi ya SIDO mkoa wa Singida iliyopo Utemini mjini Singida.

SHIRIKA la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) mkoani Singida limetoa mikopo mbali mbali yenye thamani ya zaidi ya shilingi 966.1 milioni kwa wafanyabiashara 1,326, katika kipindi cha mwaka jana.

Hayo yamesemwa hivi karibuni na Meneja Mikopo wa SIDO mkoa wa Singida, Reben Mwanja wakati akizungumza na Mwandishi wa habari hizi ofisini kwake, juu ya maendeleo ya utoaji wa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo.

Amesema kati ya fedha hizo, shilingi 457,000,000 zilitolewa kwa wakopaji/wanachama 1,0104 wa vikundi vya (solidality group), VICOBA na benki za jamii vijijini na vikundi hivyo vilikuwa 45.

“Pia shilingi 509,150,000/= zilitolewa kwa wakopaji mmoja mmoja wapatao 312. Mikopo hiyo, lengo lake ni kuwaendeleza wafanyabiashara wadogo wadogo na wa kati na sekta ya viwanda”,amesema Mwanja kwa kujiamini.

Akifafanua zaidi, Mwanja amesema kuwa kati ya wateja 1,326 walionufaika na mikopo hiyo mwaka jana, wanawake walikuwa 717 na wanaume ni 609.

Aidha,meneja huyo amesema mikopo hiyo ilitolewa katika wilaya zote za mkoa wa Singida na kwamba  imewanufaisha wafanyabiashara wadogo,viwanda, uvuvi, ufugaji na wachimbaji wadogo wadogo.

Kuhusu marejesho,Mwanja amesema kuwa marejesho ya mikopo ni asilimia 98 na kwa ujumla,hayasumbui wakopaji wanarudisha bila shida kubwa.

“Marejesho hayo mazuri, yanachangiwa kwa kiwango kikubwa na utoaji mafunzo kabla mhusika hajapewa mkopo, na vile vile usimamizi wa karibu na uendeshaji wa biashara”,amesema Mwanja.

Wakati huo huo, Meneja Mwanja amewashauri

Monday, January 27, 2014

Mvua ya mawe yaharibu ekari 800 za mazao mbalimbali Ikungi.


Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Hassan Tati akikagua mashamba ya mazao mbali mbali yaliyoharibiwa na mvua kubwa ya mawe na upepo mkali iliyonyesha juzi katika kijiji cha Siuyu.Jumla la ekari zai ya 800 zilimeharibiwa na mvua hiyo.

ZAIDI ya ekari 800 za mazao mbalimbali yaliyolimwa katika vitongoji vinne vya kijiji cha Siuyu tarafa ya Mungaa wilaya ya Ikungi,zimeharibiwa vibaya na mvua kubwa ya mawe na iliyoambatana na upepo mkali.

Hayo yamesemwa hivi karibuni na Afisa Mtendaji wa kijiji cha Unyankhanya wilaya ya Ikungi,Adriano Herman wakati akitoa taarifa ya uharibifu mkubwa wa mazao kwa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ikungi,Hassan Tati.

Amesema mvua hiyo iliyonyesha juzi usiku kuanzia saa 1.30 jioni hadi saa 2.48 usiku pia ilisababisha nyumba tatu kuanguka chini.

“Mvua hii ilionyesha mapema kwamba sio ya kheri kutokana na upepo wake kuwa mkali mno.Pia ilidondosha mabonge makubwa ya barafu ambayo yalichukua siku nzima kuyeyuka.Kwa ujumla imeharibu ekari 843,213 ya mazao mbalimbali”,amesema.

Herman alitaja mazao yaliyoharibiwa na ekari zake kwenye mabano kuwa ni viazi vitamu (12),mtama (262),uwele (93),alizeti (37.5),maharage (92.5),mahindi (137),ulezi (201.5) na karanga (7.5).

Pamoja na kuwapa pole wakazi hao,Mwenyekiti Tati aliwahakikishia kuwa halmashauri ya wilaya ya Ikungi,inafanya maandalizi ya kuwasaidia mbegu bora za mazao yanayokomaa kwa muda mfupi.

Aidha, Tati amewataka kuendelea kufuata masharti na ushauri wa watalaam wa kilimo ili waweze kupata mavuno ya kukidhi mahitaji.


“Nitumie fursa hii

Watu wasiofahamika wamnyang’anya bunduki Mzee wa miaka 71.

Kamanda wa Polisi, mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake.

WATU wasiofahamika idadi na makazi yao,wamevamia nyumba ya Daudi Karata (71) mkulima na mkazi wa kijiji cha Nguamghanga tarafa ya Mgori wilaya ya Singida mkoa wa Singida,na kunyang’anya bunduki aina ya shot gun na risasi zake nne.

Kabla na kufanya unyang’anyi huo,kundi hilo la watu wasiofahamika,lilimkata kata mapanga mzee Karata  sehemu mbalimbali za mwili kwa lengo la kufanikisha azma yao kwa urahisi zaidi.

Kamanda wa Polisi, mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela amesema tukio hilo limetokea januari 21 mwaka huu saa tano asubuhi huko katika kijiji cha Nduamghanga tarafa ya Mgori.

Amesema mzee huyo Karata,alipatiwa matibabu katika kituo kidogo cha kutolea huduma za afya kilichoandaliwa kwa muda kijijini hapo.

“Jeshi la polisi linaendelea na msako mkali ili kuwakamata watu hao na kuwafikisha mahakamani.Pia linatoa wito kwa raia wema kutoa taarifa pindi wapatapo taarifa zo zote juu ya tukio hilo”,amesema kamanda Kamwela.

Habari kutoka kijiji hicho cha Nduamghanga,zinadai kwamba baada ya mzee Karata kunyang’anywa bunduki yake shot gun,saa mbili baadaye,kundi la watu zaidi ya 300 wakazi wa kijiji cha Handa wilaya ya Nchemba mkoa wa Dodoma,walivamia kijiji hicho huku wakiwa wamebeba mapanga,rungu,pinde na bunduki moja.

Kundi hilo linadaiwa

Wednesday, January 22, 2014

Vyama vya soka mikoani vyatakiwa kukuza vipaji vya vijana.

 Makamu rais TTF Taifa,Wallace Karia (wa tatu kulia) akiwa kwenye meza kuu pamoja na viongozi wanzake muda mfupi kabla hajafungua mafunzo yaliyohudhuriwa na viongozi wa TFF mikoa mbalimbali hapa nchini jana (18/1/2014).Kulia ni katibu TFF mkoa wa Singida,Hussein Mwamba,anayefuatia ni mwenyekiti TFF mkoa wa Singida, Baltazar Kimario.Wa tatu kushoto  ni Nasibu Ramadhani mjumbe wa kamati ya utendaji TFF taifa na wa pili kushoto ni Wilfred Kidau,mjumbe wa kamati ya utendaji TFF taifa.Mada zilizotolewa kwenye mafunzo hayo ni utawala,ukaguzi wa taarifa za fedha na maendeleo ya timu ya soka ya vijana.
Makamu rais wa TFF taifa,Wallece Karia, akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili yanayoendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa Katala hotel beach iliyopo mjini Singida.

VYAMA vya soka mikoani vimetakiwa kuweka mikakati madhubuti itakayosaidia kuwajengea vijana mazingira mazuri ya kuibua vipaji vyao ili waweze kuendelezwa kwa lengo la kupata timu bora ya Taifa stars.

Hayo yanasemwa hivi karibuni na Makamu Rais wa TFF taifa,Wallace Kiria,wakati akifungua mafunzo ya siku mbili yaliyohudhuriwa na viongozi wa TFF kutoka mikoani yanayofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Katala Hotel Beach mjini hapa.Mafunzo hayo yalihusu utawala,ukaguzi wa taarifa za fedha na maendeleo ya soka la vijana.

Kiria amesema vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini wenye vipaji vya soka wakiendelezwa,watasaidia kuunda timu bora ya Taifa stars itakayokuwa na uwezo wa kutoa  ushindani wa kweli na sio ya kusindikiza.

 “Watanzania wamechoka au wamechoshwa na mwenendo wa Taifa stars wa kila inaposhiriki mashindano yoyote inatolewa mapema uongozi huu mpya wa TFF malengo yake ni kuona Taifa stars inayotoa ushindani wa hali ya juu na ikiwezekana ianze kuleta makombe mbalimbali nchini mapema”,amesema.

Aidha,Karia amesema kuwa maandalizi hayo ya kuendeleza vijana hasa chini ya miaka 17,ni kuandaa mapema timu ya vijana ambayo itashiriki mashindano ya bara hili la Afrika ambayo, Tanzania itaomba mashindano ya mwaka

Tuesday, January 21, 2014

Rais Kikwete aomboleza vifo vya watu 13 waliofariki kwenye ajali mkoani Singida.



Gari aina ya Noah T,730 BUX linavyoonekana baada ya kugongwa na Lori mkoani Singida.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mheshimiwa Perseko Kone kutokana na vifo vya watu wazima 12 na mtoto mmoja wa miezi minne vilivyotokea tarehe 20 Januari, 2014 kufuatia kugongana uso kwa uso kwa gari aina ya Toyota Noah lililokuwa limebeba abiria likitokea Itogi kwenda Singida na lori katika eneo la Isuna Mkoani Singida.

“Nimeshtushwa, nimesikitishwa na kuhuzunishwa mno na taarifa za vifo vya watu 13 akiwemo mtoto wa miezi minne waliofariki papo hapo katika eneo la ajali tarehe 20 Januari, 2014 baada ya gari aina ya Toyota Noah walilokuwa wakisafiria kutoka Itigi kwenda Singida kugongana uso kwa uso na lori katika eneo la Isuna”.

Rais Kikwete amesema inatia simanzi kuona ajali zikiendelea kutokea na kupoteza maisha ya watu wasio na hatia na hususan mtoto mdogo kama huyu wa miezi minne, kusababisha ulemavu wa kudumu kwa baadhi ya watu na uharibifu wa mali kutokana na makosa ya binadamu katika uendeshaji wa vyombo vya moto.

“Kufuatia ajali hiyo ya kusikitisha, ninakutumia wewe Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mheshimiwa Perseko Kone salamu zangu za rambirambi kutokana na msiba huo, na kupitia kwako, naomba unifikishie salamu zangu za rambirambi na pole nyingi kwa familia zote zilizopoteza wapendwa wao katika ajali hiyo. Nawaomba wanafamilia wawe na moyo wa uvumilivu, subira na ujasiri hivi sasa wanapougulia machungu ya kupotelewa na ndugu zao”, amesema Rais Kikwete kwa masikitiko.

Aidha Rais Kikwete amesema anamuomba

Ajali yaua 13 wakiwemo wa Familia moja Singida.




 Gari aina ya Noah T,730 BUX linavyoonekana baada ya kugongwa na Lori.
ABIRIA 13 wakiwemo watatu wa familia moja wamefariki dunia mkoani Singida leo, baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Noah T.730 BUK, kugongwa na Lori aina ya Scania.

Ajali hiyo ya kusikitisha imetokea leo saa  1.32 asubuhi katika barabara kuu ya Singida-Dodoma eneo la kijiji cha Isuna tarafa ya Ikungi wilaya ya Ikungi mkoani Singida.

Kamanda wa polisi mkoa wa Singida,SACP ,Geofrey Kamwela, amesema gari hilo aina ya Noah lilikuwa likitokea Itigi wilaya ya Manyoni na lilikuwa na safari ya kuja Singida mjini.

Amesema hadi sasa miili ya abiria 10 wamekwisha tambuliwa na ndugu zao na miili ya abiria watatu,bado haijatambuliwa na miili yote bado imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia  maiti cha hospitali ya mkoa mjini Singida

Alitaja waliotambuliwa na makazi yao kwenye mabano kuwa ni Omari Shaban (44) na mke wake Salma Omari  na mtoto wao Nyamumwi Omari (10) wote wakazi wa Itigi mjini.

Kamwela alitaja wengine kuwa ni Haji Mohammed (29) (Msisi),Mtunku Rashidi (68) (Sajaranda),Salehe Hamisi (28) (Sajanranda),Samir Shaban (20) (Puma),Mwaleki Nkuwi (35) (Ikungi),Athumani Kalemba (38) na Ramadhan Mkenga (Sajaranda).Katika ajali hiyo,abiria watatu walinusurika na kupata majeraha madogo madogo.

Amefafanua juu ya ajali hiyo,Kamanda huyo alisema kuwa lori aina ya scania T.687 AXB wakati likipishana na noah,lilihama upande wake na kuifuata noah ambayo ilikuwa upande wake wa kushoto,na kuligonga na kisha kuliburuza kati zaidi ya 15.

“Kwa sasa bado hatujajua chanzo cha ajali hiyo mbaya ingawa baadhi ya watu wanadai kuwa huenda

Monday, January 20, 2014

PICHA KUMI (10) ZA AJILI MBAYA ILIYOTOKEA SINGIDA NA KUUWA WATU 13 PAPOHAPO.

TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI KAMA ZITAKUKWAZA.
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Isuna tarafa ya Ikungi wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, wakitoa miili ya abiria wa Noah T.730 BUX waliofariki baada ya gari hilo kugongwa na lori aina ya Scania T.687 AXB kwenye barabara kuu ya Singida – Dodoma leo


Baadhi ya miili ya abiria wa Noah T,730 BUX waliofariki leo kwenye ajali iliyotokea eneo la kijiji cha Isuna tarafa ya Ikungi wilaya ya Ikungi.

Mtoto aibiwa katika mazingira ya kutatanisha.

Kamanda wa polisi mkoani Singida, SACP Geofrey Kamwela, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na tukio la kupotea kwa mtoto.

MTOTO Meristina Samwel mwenye umri wa mwezi mmoja na siku moja mkazi wa Misuna Manispaa ya Singida ameibiwa katika mazingira ya kutatanisha.

Kamanda wa polisi mkoani Singida, SACP Geofrey Kamwela amesema tukio hilo la wizi wa mtoto, limetokea Januari 14 mwaka huu saa tano asubuhi huko katika mtaa wa Ginery kata ya Mandewa tarafa ya Unyakumi Manispaa ya Singida.

Amesema siku moja kabla ya tukio, mwanamke ambaye jina lake bado halijafamika, alifika Misuna nyumbani kwa mama wa mtoto aliyeibiwa, aitwaye Fatuma Jumanne (26) na kudai anatafuta mtoto wa kazi.

 “Baada ya mazungumzo ya muda kati ya wanaweke hao, kulijengeka aina fulani ya urafiki uliopelekea mwanamke mwizi wa mtoto kurudi tena  nyumbani kwa Fatuma”,amesema.

Kamwela amesema siku hiyo januari 14 saa tano asubuhi, mwanamke huyo, akiwa nyumbani kwa Fatuma alimwombwa mwenyeji wake waende wote Ginery ili akamwonyeshe nyumbani kwake.

Akifafanua zaidi, amesema kwa vile Fatuma alikuwa na watoto wawili, yule mwanamke mwizi, aliomba kubeba mtoto mchanga na Fatuma akabeba yule mkubwa.

 “Walipofika Ginery, mwanamke mwizi alimpeleka Fatuma mgahawani akamnunulia

Diwani wa CCM mbaroni kwa kuchoma basi la Mtei.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela.

DIWANI wa kata ya Umyambwa tarafa ya Mungumaji Halmashauri ya Manispaa ya Singida,(CCM) Shaban Satu na watu wengine tisa,wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma ya kuchoma moto basi la kampuni ya Mtei Express ya mjini Arusha.

Diwani huyo na wapiga kura wake,inadaiwa kulichoma moto basi hilo januari tisa mwaka huu saa moja na dakika moja barabara ya Singida-Arusha eneo la kijiji cha Kisasida manispaa ya Singida.

Watuhumiwa hao walifikia uamuzi huo kutokana na basi hilo T.742 ACU lililokuwa linaendeshwa na Dismas Ludovick, kugonga bodaboda T.368 BXZ iliyokuwa imepakia watu wanne wa familia moja.

Wanafamilia hao ambao walikuwa wakienda shamba,ni Tamili,Kassim na Hamza ambao ni watoto wa Shabani Bunku ambaye alikuwa akiendesha bodaboda hiyo.Watoto wote watatu walipoteza maisha na baba yao bado anaendelea na matibabu katika hospitali ya misioni ya Hydom mkoani Manyara.

Kamanda wa polisi mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela,amekiri diwani huyo na wapiga kura wake

Abiria 48 wanusurika kufa kwenye ajali ya basi la Shabiby.

 Mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi (mbele ya basi lililopinduka aliyenyoosha mkono) akiangalia basi la Shabiby lililopinduka eneo la kijiji cha Kisaki manispaa ya Singida.Basi hilo ambalo lilijeruhi abiria 28 akiwemo kondakta aliyevunjika miguu yote, lilipinduka katika harakati zake za kulipita basi jingine.
 Lori la mafuta lililogongwa na basi la Shabiby na kusababisha abiria 28 kujeruhiwa.
Kondakta wa basi la shabiby Tadei Mhando aliyevunjika miguu yote miwili baada ya basi hilo kupinduka eneo la kijiji cha Kisaki manispaa ya Singida. Waauguzi wa hospitali ya mkoa mjini hapa,wakimpeleka kondakta Tadei Mhando chumba cha upasuaji.

ABIRIA 48 wa basi la kampuni ya Shabiby lifanyalo safari zake kati ya mkoa wa Arusha na Dodoma, wamenusurika kufa baada ya basi hilo kupinduka wakati likijaribu kupita basi jingine.

 Basi hilo aina ya Yutong lenye namba za usajili T.930 BUW, limepinduka katika barabara kuu ya Singida-Dodoma eneo la kijiji cha Kisaki Manispaa ya Singida.

 Ajali hiyo imetokea saa saba mchana wakati basi hilo likitokea mkoani Arusha kuelekea mjini Dodoma.

 Kondakta wa basi hilo,Tadei Mhando amesema kati ya abiria hao,28 wakiwemo watoto wawili,wamepata majeraha katika sehemu zao mbalimbali za miili yao.

 “Mimi ndiye niliyeumia zaidi kuliko majeruhi wote wa basi letu.Nimevunjika miguu yote miwili na sasa natarajia kuingizwa ‘theater’ kwa matibabu zaidi.Tunashukuru hakuna mtu aliyepoteza maisha”,amesema Tadei.

 Akifafanua zaidi juu ya ajali hiyo,Tadei amesema walipofika eneo la tukio la Kisaki ambalo lina mwiinuko huku basi lao likiwa kwenye mwendo kasi,dereva wao alijaribu kulipita basi la Princess Muna.

Amesema katika jaribio hilo,mabasi yote mawili yakawa kwenye mwendo kasi unaofanana na wakati huo huo,

Friday, January 10, 2014

Watu watatu wa familia moja wamefariki dunia baada ya kugongwa na basi la Mtei Express.

Basi la kampuni ya Mtei Express T.742 ACU linavyoonekana baada ya kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali wa kitongoji cha Ijanuka kijiji cha Kisasida manispaa ya Singida,kutokana na kugonga pikipiki aina ya sky go T.368 BXZ na kuua abiria watatu waliokuwa kwenye pikipiki hiyo.Basi hilo lilikuwa likitoka Singida mjini kuelekea Arusha mjini leo.

 WATU watatu wa familia moja wamefariki dunia baada ya pikipiki waliyokuwa wakisafiria kugongwa na kuburutwa na basi la kampuni ya Mtei Express ya mjini Arusha.

Watu hao ni Tamili Shaban na Kassimu wamefariki dunia papo hapo kwenye eneo la tukio ambalo ni kitongoji cha Ijanuka kijiji cha Kisasida Manispaa ya Singida.Hamza amefariki dunia akiwa anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa mjini Singida.Miili ya watu hao imehifadhiwa katika chumba cha mochwari katika hospitali ya mkoa.


Baba mzazi wa watoto hao,Shaban Bunku ambaye imedaiwa ni mlinzi wa kampuni ya TTCL mjini hapa,amelazwa katika hospitali ya mkoa na hali yake ni mbaya.Inadaiwa kuvunjika mguu wa kulia na damu zilikuwa zikimtoka kichwani.

Wanafamilia hao wanadaiwa walikuwa wakienda shamba kuendelea na palizi.

Akizungumzia tukio hilo la kusikitisha,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela amesema tukio hilo limetokea leo saa moja na dakika moja asubuhi huko katika kitongoji cha Ijanuka kijiji cha Kisasida.

Amesema siku ya tukio,basi la kampuni ya Mteni lenye namba za usajili T.742 ACU aina ya scania likiendeshwa na Dismas Ludovick,lilikuwa linatokea Singida mjini likielekea Arusha mjini.

Kamwela amesema lilipofika kitongoji cha Ijanuka,kwa  pikipiki aina ya sky go T.368 BXZ iliyokuwa inaendeshwa na Shaban Bunku huku akiwa amepakia watoto wake wa kiume watatu,ilikatisha ghafla kitendo kilichosababisha kugongwa na kuburutwa zaidi ya hatua 20.

“Dereva wa basi hilo ambalo lilikuwa na abiria tisa,alilazimika kusimamisha basi hilo kutokana na kuburuta pikipiki hiyo.Baada ya kusimamisha basi hilo,wananchi wa eneo hilo walipigiana simu na ghafla walijaa na kuanza kuvunja vunja vyoo na kisha kilichoma moto”,amesema Kamwela.

Wakati huo huo,Kamanda Kamwela amesema wameanzisha msako mkali wa kusaka

Akamatwa na noti bandia zaidi ya shilingi 3.4milioni.

 Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela.
 
JESHI la Polisi Mkoani Singida linamshikilia mfanyabiashara mmoja kwa tuhuma za kupatikana na noti bandia za shilingi 10,000 na 5,000 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 3.4 milioni

 Mtuhumiwa huyo Toye Wagela (39) mkazi wa kijiji cha Mitale mkoa wa Kigoma amekamatwa juzi saa nane mchana wakati akijaribu kununua chakula kwenye hotel moja wilayani Manyoni Mkoa wa Singida.

 Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela amesema kuwa baada ya mtuhumiwa kutoa moja ya noti hizo na kutiliwa shaka alianza kujaribu kukimbia kabla ya kukamatwa na wananchi.

 Amesema kuwa wananchi hao waliita polisi ambapo baada ya kupekuliwa kwenye mifuko ya suruali, mtuhumiwa alikutwa na noti 200 za shilingi 10,000 na nyingine 209 za shilingi 5,000.

 Kamanda Kamwela amesema wanaendelea kufanya uchunguzi wa kina na kuwatafuta washirika wengine wa uhalifu huo,kabla ya mtuhumiwa kupandishwa  kizimbani kujibu tuhuma ya kupatikana na noti bandia.

Thursday, January 9, 2014

Wanafunzi bora wa masomo ya sayansi waenda Ireland.

Mwakilishi  kutoka  Ubalozi wa Ireland nchini, Rita Bowen (wa pili kushoto) akikabidhi zawadi kwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ilongelo  ya Singida, Jafari Ndagula mmoja wa washindi wawili wa jumla wa  shindano la Wanasansi Chipukizi Tanzania 2013 (YST) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Jafari na mwenzake Fidel Samwel (hayupo pichani) wataiwakilisha Tanzania katika sherehe za  Tuzo  za kimataifa za wanasayansi chipukizi duniani mjini Dublin Ireland. Tuzo za YST  zinadhaminiwa na Ubalozi wa Ireland kwa kushirikiana na Mfuko wa Karimjee Jivanjee Foundation (KJF). Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa YST, Dk. Gosbert Kamugisha na Mwenyekiti wa Mfuko wa KJF, Hatim Karimjee.

SHIRIKA la Irish Aid kwa kushirikiana na Taasisi ya Karimjee Jivanjee “KJF” kwa kufadhili wanafunzi wanne bora toka shule ya sekondari ya Ilongero ya Singida na Fidel Castro ya Pemba kwenda Dublin, Ireland baada ya kuibuka washindi wa jumla katika mashindano ya wanasayansi chipukizi (Young Scientists Tanzania) YST mwaka 2013.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa udhamini na kuwaaga rasmi wanafunzi wao jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Taasisi ya karimjee Jivanjee, Hatim Karimjee amesema kwamba wanafunzi wawili  kutoka shule ya sekondari ya Ilongelo, Jafari Ndagula na Fidel Samwel walishinda tuzo za jumla katika mashindano ya YST 2013 kwa kufanya utafiti wa mradi wa kilimo cha umwagiliaji kwa njia ya kutumia matone (Recycled Material)

“washindi walipokea zawadi ya fedha taslimu, medali, laptops na sasa ziara ya kwenda Dublin Ireland kuwawakilisha wanafunzi wa kitanzania katika sherehe za kimataifa za wanasayansi chipukizi duniani,” amesema karimjee

“Washindi pia walipata udhamini kutoka Karimjee Jivanjee Foundation kwa ajili ya masomo yao ya chuo kikuu kwa siku zijazo kama sehemu ya jitihada za msingi za kusaidia maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika nchi ya Tanzania,” alilisitiza.

 Amesema kuwa YST pia iliwapa tuzo wanafunzi wawili , Muslih Othman Khamis na Amne Said Sauti kutoka shule ya Sekondari ya Fidel Castro kutoka Pemba kwa ajili ya utafiti wao wa kisayansi juu ya (ethanol) kwa kutumia miwa.

“matokeo ya utafiti wao yatasaidia kupunguza uharibifu wa mazingira kwa watu badala ya kutumia kuni au mkaa au kutumia pesa nyingi kununua mafuta ya taa, wanaweza kutumia ethanol iliyotengezwa kutokana na miwa ambayo inapatikana kwa wingi huko Pemba,” amesema

” KJF wamekuwa wakisaidia YST tangu 2012 na kuwa mdhamini mkuu na mwaka 2013 KJF waliongeza msaada wake kwa YST kwa kutoa udhamini kwa washindi wa ujumla ikiwa ni pamoja na masomo ya juu kwa ajili ya wale wanaohitaji,” aliongeza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ofisi ya Kamishina wa Elimu, Hadija Mcheka amesema kuwa serikali inaunga mkono kwa ukamilifu mpango ulioanzishwa na YST kwa sababu itaweza kukuza na kuhamasisha wanafunzi kujiingiza katika masomo ya sayansi.

 ”Programu  Hii itakuwa inakuza na kuhamasisha ubunifu miongoni mwa wanafunzi katika nchi wakati jukwaa hili pia litasafisha njia kwa ajili ya wanafunzi kuja pamoja na na kubadilishana uzoefu, ” alieleza.

YST Mkurugenzi Dk Gosbert Kamugisha amesema kuwa waliamua kuja na mpango huo kutokana na ukweli kwamba matokeo ya kidato cha nne na sita kwenye masomo ya sayansi yalikuwa yakishuka siku hadi siku.

Amesema, ” YST ” iliwakutanisha wanafunzi 120 na 60 kutoka shule za sekondari katika mikoa ipatayo 18 na mashindano hayo yalifanyika

Wadau wa Afya Singida waridhia mpango wa Tiba kwa kadi.

Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Vicent Kone akizungumza kwenye uzinduzi wa mpango wa Tiba kwa kadi (TIKA) katika halmshauri ya manispaa ya Singida uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Aque Vitae Resort mjini Singida. Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Singida, Queen Mlozi.
 Meneja msaidizi wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoa wa Singida, Isaya Shekifu, akizungumza muda mfupi kabla ya kumkaribisha mkuu wa mkoa wa Singida.Dk.Parseko Kone, kuzindua mfuko wa Tiba kwa kadi (TIKA) katika manispaa ya Singida. Walioketi kutoka kulia ni mkuu wa wilaya ya Iramba,Yahaya Nawanda na Mstahiki Meya wa manispaa ya Singida,Sheikh Salumu Mahami.
 Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoa wa Singida,Yahaya Nawanda, akitoa mada yake iliyohusu mfuko wa afya ya jamii (CHF) kwenye mkutano wa wadau wa afya wa manispaa ya Singida.
Mkuu wa wilaya ya Singida,Queen  Mlozi,(wa kwanza kulia) akisikiliza mada zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano wa wadau wa afya wa manispaa ya Singida. Wa kwanza kushoto,ni mstahiki meya wa manispaa ya Singida,Sheikh Mahami.
Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone (wa tatu kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na madiwani wa manispaa ya Singida.Walioketi wa  kwanza kulia ni Diwani wa viti maalum Yagi Kiaratu na anayefuatia ni mstahiki Meya wa manispaa ya Singida,Sheikh Salum Mahami.Kulia ni Katibu Tawala mkoa wa Singida,Liana Hassan mkuu wa wilaya ya Iramba,Yahaya Nawanda na mkuu wa wilaya ya Iramba na Queen Mlozi, mkuu wa wilaya ya Singida.

WADAU wa afya katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida kwa kauli moja wameridhia kuanzishwa kwa Mpango wa Tiba kwa Kadi (TIKA) katika Manispaa hiyo.

 Wadau hao wamefikia uamuzi huo baada ya kubaini kuwa mpango wa TIKA una manufaa mengi ikiwemo mwananchi baada ya kulipa ada ya uanachama, atakuwa na haki ya kupata huduma za matibabu ndani ya Manispaa kwa mwaka mzima.

 Kwa mujibu wa Meneja Msaidizi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Singida, Isaya Shekifu mpango wa TIKA ambao unafafana na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) unatumika mijini tu.

 Shekifu amesema uanachama wa TIKA ni wa mtu mmoja mmoja, wakati ule wa CHF, ni wa familia au kikundi.

 “Kwa sasa hapa Manispaa ya Singida, baada ya mpango huo kupata baraka ya kuanzishwa tunaendelea na mchakato wa kubadilisha sheria ndogo ya CHF kwenda kwenye Tiba kwa Kadi (TIKA)”,alifafanua Shekifu.

 Meneja Msaidizi huyo amesema baada ya kukamilika kwa sheria ndogo itakayotawala uendeshaji wa TIKA, mpango huo utaanza rasmi mapema iwezekanavyo mwaka huu.

 Akizindua mpango huo wa Tiba kwa Kadi (TIKA) katika Manispaa ya Singida juzi, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone amesema mpango wa TIKA utawahakikisha wakazi wa Manispaa ya Singida na viunga vyake  mwanzo mpya wa kupata huduma za matibabu zenye uhakika.

 Hata hivyo, Dk. Kone aliagiza  viwango vya uchangiaji vya TIKA zitazingatia uwezo wa mwananchi kulipia pia vitazingatia

Mke amuua mume kwa kumpiga na kipande cha Mti Kichwani kisa Tsh. 25,000/=

Kamanda wa polisi mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela,akitoa taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) juu ya kifo cha Mwanaume aliyeuwawa na mkewe kwa kupigwa na kipande cha mti kichwani.

MKULIMA na Mkazi wa kijiji cha Ntewa, Kata ya Ntuntu tarafa ya Munghaa wilaya ya Ikungi mkoani Singida,Juma Abdallah (25) amefariki dunia baada ya kupigwa na mke wake Veronika Hamisi (25) kichwani katika paji la uso na na kufariki papo hapo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela amesema tukio hilo limetokea januari  mbili mwaka huu saa saba mchana huko katika kijiji cha Ntewa.

Amesema siku ya tukio katika muda huo wa saa saba mchana wanandoa hao walirejea nyumbani kwao wakitokea kwenye klabu cha pombe za kienyeji aina ya mtukuru.

“Wanandoa hao vijana wakiwa nyumbani kwao,Juma alichukua pochi ya mke wake Veronica na kuchukua bila idhini shilingi 25,000 zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye pochi hiyo”,amesema.

Kamanda Kamwela amesema baada ya Juma kuchukua fedha hizo bila idhini mke wake alimsihi sana azirudishe fedha hizo mahali zilipokuwa lakini juhudi hizo hazikuzaa matunda.

“Hata hivyo,Veronica alipoona juhudi zake zimegonga mwamba aliita wanaume wawili ambao majina yao hayajajulikana.Wanaume hao walipomshika Juma hapo ndipo Veronica alipopata fursa ya kuchukua kipande cha mti na

Wakazi wa Singida wakumbushwa umuhimu wa elimu kwa maendeleo yao.

Mkurugenzi wa chuo kikuu huria tawi la mkoa wa Singida, Bw. Mbaraka Msangi, akitoa taarifa yake kwenye sherehe za kuwapongeza wahitimu 52 wa chuo hicho zilizofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kanisa Katoliki mjini Singida.
Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Paresko Vicent Kone, akizungumza kwenye kilele cha sherehe ya kuwapongeza wahitimu wa chuo kikuu huria cha mkoa wa Singida,zilizofanyika mwishoni mwa juma mjini Singida.Wa kwanza kulia ni mkurugenzi wa chuo hicho,Mbaraka Msangi.
Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone (kushoto) akimkabidhi Mwalimu Allan Jumbe cheti cha kuhitimu chuo kikuu huria mjini Singida.Kwa mwaka huu,jumla ya wanafunzi 52 wamefanikiwa kuhitimu katika chuo hicho.
Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone, (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu wa chuo kikuu huria tawi la Singida. Sherehe ya kupongeza wahitimu hao,ilifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kanisa katoliki mjini Singida.

MKUU wa Mkoa wa Singida,Dk.Parseko Vicenti Kone amewakumbusha wakazi wa mkoa huo umuhimu wa kujiunga na chuo kikuu huria tawi la mkoani humo ili kujiendeleza kielimu.

Amesema kujiendeleza kielimu kutasaidia mhusika kujijengea mazingira mazuri ya kumudu maisha yake kwenye dunia hii iliyojaa ushindani wa kila aina.

 Dk.Kone ametoa wito huo hivi karibuni wakati akizungumza kwenye hafla fupi ya kuwapongeza wahitimu wa chuo kikuu huria kituo cha mkoa wa Singida wa mwaka jana.

 Amesema changamoto zinazojitokeza hivi sasa Tanzania,Afrika mashariki na duniani kwa ujumla pamoja na maendeleo ya kisayansi na teknolojia zinatulazimisha sisi wote kuwa na elimu ya kutosha ili kuzikabili.

 “Watanzania tusipokuwa na elimu ya kutosha tutaachwa mbali sana na wenzetu wa nchi zinazotuzunguka na wa dunia kwa ujumla.Tusisubiri jambo hili likatokea ili hata jumuiya ya Afrika mashariki itakapokamilika tusije tukakuta nafasi nyingi za kazi zinachukuliwa na wenzetu badala ya vijana wetu,alifafanua Mkuu huyo wa mkoa.

 Dk.Kone amesema kutokana na ukweli huo wazazi na walezi wanalo jukumu la kuwashauri na kuwahimiza vijana wao kujiendeleza kwa nguvu zote ili kupata elimu inayokidhi mahitaji ya sasa na yajayo.

 Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa mkoa amewataka kupuuza dhana potofu kuwa elimu inayotolewa na chuo kikuu huria siyo ya kiwango cha juu bali ni ya kihuria huria tu.

 “Dhana hii potofu inayoenezwa kwa lengo la kuwakatisha tamaa Watanzania walio wengi wasipate