Thursday, October 31, 2013

Shule ya msingi Ikungi yazindua ufundishaji kwa njia ya TEHAMA.

Mkuu wa wilaya ya kungi mkoani Singida, Manju Msambya akizindua mitambo ya kufundishia kwa njia ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) katika shule ya msingi Ikungi mchanganyiko.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi (mwenye skafu) akipewa maelezo na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ikungi mchanganyiko, Olivary Kamili,juu ya mitambo ya kufundishia TEHAMA.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Manju Msambya akiangalia screen inayoonyesha namna somo linavyotolewa kupitia TEHAMA.

Shule ya Msingi Ikungi mchanganyiko wilaya ya Ikungi mkoani Singida imezindua rasmi ufundishaji wa kisasa kupitia mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kuwawezesha wanafunzi kutumia vifaa mbalimbali katika mawasiliano na kujiendeleza kielimu.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo,Mwalimu Mkuu wa shule hiyo,Olivary Kamili amesema mfumo huo wa ufundishaji pia utawawezesha wanafunzi kwenda na wakati katika kujifunza.

Akifafanua amesema mfumo huo utawajengea mazingira mazuri wanafunzi kuwa na tabia ya udadisi ambayo itapelekea wawe wagunduzi.

“Kupitia somo la TEHAMA wanafunzi watajenga tabia ya kujifunza kupitia udadisi wa mambo mbali mbali hivyo itasaidia kupata vijana ambao watakuwa na uwezo wa kufanya tafiti za uhakika”,amesema Mwalimu Kamili.

 Aidha, amesema kutokana na umuhimu wa somo la TEHAMA ameishauri Serikali ilipe kipaumbele kwa kuhakikisha shule zote zinanufaika na somo hilo.

 “Somo la TEHAMA linarahisisha sana upatikanaji wa elimu bora na yenye mafanikio makubwa.Napendekeza serikali iangalie namna ya kuboresha somo hili ili liweze kuwa na

Wednesday, October 30, 2013

Kero za wananchi zinahitaji majadiliano ya pamoja.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi, Protace Magayane akizungumza kwenye mahafali ya 13 ya shule ya sekondari Sepuka.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi, Protace Magayane (mwenye miwani) akimkabidhi cheti cha kuhitimu kidato cha nne mmoja kati ya 58 wa shule ya sekondari Sepuka.

Baadhi ya wazazi/walezi wa wanafunzi wanaotarajiwa kumaliza kidato cha nne mwaka huu wa shule ya sekondari ya Sepuka wilaya ya Ikungi.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Protace Magayane amewahimiza wazazi  na walezi kujenga utamaduni wa kujadili kwa pamoja kero zinazowakabili katika maeneo yao na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.

Magayane ametoa changamoto hiyo hivi karibuni wakati akizungumza kwenye kilele cha mahafali ya 13 ya shule ya sekondari ya Sepuka, Jimbo la Singida Magharibi.

Akifafanua amesema katika mikutano ya kitongoji, Kijiji na Kata wananchi hawana budi kuweka bayana kero na shida zao na kuzipa vipaumbele.

Akitoa mfano, Magayane amesema katika majadiliano hayo ya pamoja, wanaweza kubainisha kero zinazowakabili katika sekta mbalimbali zikiwemo za sekta ya barabara, maji, elimu na afya.

“Wananchi kwa ushirikiano na viongozi wenu,baada ya kujadiliana,muweke mikakati ya pamoja ya namna ya kutumia nguvu zenu wenyewe katika kutatua kero hizo”,alifafanua Mkurugenzi huyo.

Aidha amewataka katika majadiliano hayo waweke utaratibu wa matumizi bora ya raslimali za ardhi, maliasili, madini na zinginezo ili

Diwani wa Chadema kizimbani kwa kuvunja ofisi ya kijiji na kuiba.

Diwani wa CHADEMA kata ya Iseke jimbo la Singida magharibi Emmanuel Jackson Jingu (45) akiwa kwenye chumba cha mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida, akisubiri kusomewa kesi yake ya kuvunja na kuiba kwenye ofisi ya serikali ya kijiji cha Nkhoiree.Diwani Emmanuel alishinda nafasi hiyo hivi karibuni kwenye chaguzi ndogo zilizofanyika hivi karibuni.

Diwani wa Kata ya Iseke Tarafa ya Ihanja (CHADEMA) Jimbo la Singida Magharibi, Emmanuel Jackson Jingu (45) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Singida akikabiliwa na mashitaka mawili ya kuvunja ofisi ya kijiji cha Nkhoiree.

Mapema Mwendesha Mashitaka Mwanasheria wa Serikali, Petrida Muta alidai mbele ya Hakimu Asha Mwetindwa kuwa mnamo septemba 20 mwaka huu saa 8.30 mchana mshitakiwa alivunja nyumba kwa lengo la kuiba mali huku akijua wazi kwamba kitendo hicho ni kinyume cha sheria.

Mwendesha Mashitaka Muta alimsomea mshitakiwa shitaka la pili kuwa siku hio hiyo na wakati huo huo mshitakiwa baada ya kuvunja mlango wa nyumba inayotumiwa na serikali ya kijiji cha Nkhoiree aliweza kuiba vifaa mbalimbali vyenye thamani vya thamani ya shilingi 298,000.

Alitaja vifaa hivyo na thamani yake kwenye mabano kuwa ni vocha (hazikuweza kuelezwa ni za nini)(32,000),vitabu vya risiti (12,000),cash book (10,000),risiti za ushuru (28,000),hati za malipo (4,000),vitabu vya ushuru (10,000),risiti za zahanati (28,000) na madumu tupu 100 (150,000).

Mshitakiwa alikana mashitaka hayo na ameenda rumande baada ya kukosa mdhamini wa ahadi ya shilingi

Tuesday, October 29, 2013

UNYAMA:WANAWAKE 3 WADAIWA KUMUUA MWENZAO KWA KUDAI HAKI YA MWANAE.

Mtuhumiwa wa mauaji Tabu Jumanne (50) mkazi wa Kibaoni Singida mjini (katikati anayekwepa kamera) akiwa kwenye chumba cha mahakama ya wilaya ya Singida akisubiri kusomewa shitaka la kuumuawa Fatuma Shaban. Tabu anakabiliwa na shitaka la kumuuawa Fatuma, akishirikiana na binti zake Halima Swedi (anayejificha mwenye fulana nyekundu) na Mwamvua Yusuph baada ya mwanamke huyo kumdai Tabu amlipe mshahara binti yake aliyekuwa akifanya kazi za ndani.

Askari polisi wakiwa na mahabusu wakiwapeleka mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Singida kusomewa mashitaka yanayowakabili.

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 50 na watoto wake wawili wa kike wakazi wa Kibaoni mjini Singida wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Singida wakituhumiwa kumuuawa Fatuma Shaban maarufu kwa jina la mama Rabeca.

Washitakiwa hao ni Tabu Jumanne na binti zake Halima Swedi na Mwamvua Yusuph.

Mapema Mwendesha Mashitaka Sajenti wa Polisi Godwel Lawrance alidai mbele ya  Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Singida, Flora Ndale kuwa mnamo julai nne mwaka huu majira ya jioni huko katika kitongoji cha Mahembe kata ya Kinadi Manispaa ya Singida washitakiwa kwa pamoja walimpiga Fatuma Shaban sehemu mbalimbali za mwili wake.

Lawrance amesema kipigo hicho kilisababisha kifo cha Fatuma pale pale.

Washitakiwa hawakutakiwa kujibi cho chote kwa vile Mahakama hiyo ya Wilaya haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji Kesi hiyo inatarajiwa kutajwa tena Novemba sita mwaka huu.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa siku ya tukio Fatuma alienda nyumbani kwa mshitakiwa Tabu kudai fedha za

Wanaokataa kuchangia Maendeleo ya sekta ya Elimu ni Walemavu wa akili.

Mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi Ikungi mchanganyiko wilaya ya Ikungi,Naftali Gukwi akitoa nasaha zake kwenye ufunguzi wa sherehe ya mahafali ya 62 ya shule hiyo yaliyofanyika  mkoani Singida.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ikungi mchanganyiko,Olivary Kamili akitoa taarifa yake kwenye kilele cha mahafali ya 62 ya wahitimu 179 wa darasa la saba.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida,Manju Msambya akizungumza kwenye mahafali ya 62 ya shule ya msingi Ikungi mchanganyiko. Wa kwanza kulia ni mwenyekiti wa kijiji cha Ikungi,Machemba Mghewa na kushoto ni mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Naftali Gwae.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida,Manju Msambya, akimkabidhi cheti cha kuhitimu elimu ya msingi mmoja wa wanafunzi 179 waliohitimu.
Baadhi ya wahitimu wa wa darasa la saba wa shule ya msingi Ikungi wilaya ya Ikungi wakiwa na vyeti vyao vya kuhitimu elimu ya msingi baada ya kukabidhiwa na mkuu wa wilaya ya Ikungi,Manju Msambya.\

Wakazi wa wilaya ya Ikungi mkoani singida ambao wamekubali kudanganyika na kuamua kugoma kuchangia maendeleo yao yakiwemo ya sekta ya elimu hao ni walemavu wa akili imeelezwa.

 Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Manju Msambya, wakati akizungumza kwenye mahafali ya 62 ya shule ya msingi Ikungi mchanganyiko Jumla ya wanafunzi 179 wamehitimu elimu ya msingi.

 Amesema wilaya hiyo ya Ikungi na hasa jimbo la Singida mashariki imepandikizwa sera mbaya ya kuwataka wananchi kutokuchangia kabisa maendeleo yao.

 “hapo awali uzoefu unaonyesha wazi wananchi wakiwemo wa jimbo la Singida mashariki, walikuwa wanachangia kwa hali na mali maendeleo yao bila shuruti. Mfano mzuri ni kwamba wamejenga kwa moyo mmoja shule za sekondari za kata na zingine, kuwa na vyumba vya madarasa vya ziada.”,amesema Msambya.

 Akifafanua zaidi, DC huyo amesema baada ya sera hiyo isiyo na mashiko wala tija kupandikizwa wananchi hawataki tena kuchangia wala

Friday, October 25, 2013

MKOA WA SINGIDA WADHIBITI VITENDO VYA UHALIFU.

                                     MRAKIBU WA POLISI BW.JAMES KASUSURA

                         PICHA ZOTE TOKA MAKITABA YA SINGIDAYETUBLOG.

Mkoa wa Singida ni miongoni mwa mikoa minne nchini iliyofanikiwa kupambana na vitendo vya uhalifu kwa kiwango kikubwa kwa kipindi cha hivi karibuni.

Mrakibu  wa Polisi kutoka makao makuu Dar es salaam kitengo cha maadili James Kasusura amesema hayo wakati akizungumza na washiriki wa kikao cha siku maalum ya polisi kilichofanyika katika ukumbi wa Aquar manispaa ya Singida.

Kasusura ameyataja makosa yaliyopungua kuwa ni makosa dhidi ya ubinadamu ambayo yamepungua kwa asilimia 35, makosa dhidi ya mali yamepungua kwa asilimia 18, makosa dhidi ya maadili yamepungua kwa sailimia 13, na makosa dhidi ya usalama barabarani yamepungua kwa asilimia 12.

Amesema kupungua kwa makosa hayo kumetokana na ushirikiano baina ya raia na vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Singida, hivyo kutoa wito wa kuendelezwa kwa ushirikiano huo na hatimae kukomesha vitendo hivyo kabisa.

MSAKO MAALUM KWA WANAOISHI KINYUME NA SHERIA MKOANI SINGIDA


PICHA ZOTE NI KUTOKA MAKTABA YA SINGIDAYETUBLOG

Mkoa wa singida unatarajia kuanza operation ya ukaguzi wa kubaini watu wanaoishi nchini kinyume na sheria.
Hayo yamebainishwa jana na Afisa uhamiaji mkoa wa Singida Bw. Adam Mnyeke wakati akizungumza katika siku maalum ya polisi iliyofanyika katika ukumbi wa Aquar Manispaa ya Singida,
Bw. Mnyeke amesema kuwa zoezi hilo linatarajia kuanza wiki ijayo, hivyo kutoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa taasisi hiyo ili kupambana na wahamiaji haramu.
Amesema kwa kuanza, zoezi hilo litaanzia manispaa ya singida na baadaye litakwenda katika wilaya nyingine za mkoa wa Singida, na kuongeza kuwa zoezi hilo pia litasaidia kupambana na vitendo vya uhalifu ambavyo mara nyingi vimekuwa vikifanywa na wahamiaji haramu.

Halmashauri ya Singida kunufaika na mradi wa barabara unaofadhiliwa na benki ya dunia.


Kampuni ya Kichina ya SIETCO ikijenga kwa kiwango cha lami barabara ya Singida hadi kijiji cha Mwankoko Barabara hiyo ni moja kati ya barabara zinazojengwa kwa kiwango cha lami kwa ufadhili  wa Benki ya Dunia.

Halmashauri ya Manispaa ya Singida itanufaika na mradi wa uimarishaji na uendelezaji wa miundombinu ya barabara yenye urefu wa kilometa 15.32 kwa kiwango cha lami unaofadhiliwa na Benki ya Dunia (WB).

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida,Joseph Mchina wakati akitoa taarifa yake ya utekelezaji wa kazi za barabara kwa kipindi cha kuanzia februari hadi agosti mwaka huu.

“Jumla ya shilingi 329 milioni tayari zimekwisha tengwa kwa ajili ya kazi ya upembuzi yakinifu,uandaaji makisio na michoro ya kihandisi ya uimarishaji wa miundo mbinu ya barabara zenye urefu wa kilometa 15.32″,amesema Mchina.

Mkurugenzi huyo alizitaja barabara hizo na urefu wake wa kilometa kwenye mabano kuwa ni barabara ya Karume itakayojengwa njia mbili (0.72),Karume – Ukombozi,barabara ya Singida-Dodoma-Arusha (1.3) na barabara ya Boma-Kinyeto (2.7).

Mchina alitaja barabara zingine kuwa ni Makutano ya barabara ya Karume-Dodoma (1.6),Majengo-Karakana -shule ya viziwi(1.7),Mkutano ya barabara ya Karume-soko la zamani la vitunguu-Mwenge DP (0.5) na makutano ya barabara ya Sepuka-Airport-VETA (1.4).

“Zingine ni makutano ya barabara ya Arusha-Karakana ya ujenzi (0.3),barabara ya Semali-kituo kipya cha mabasi (1.1) na makutano ya barabara ya

Thursday, October 24, 2013

WALIOISACHI MAITI NA KUFANYA UNYANG'ANYI WAHUKUMIWA MIAKA 120 JELA.

Askari wa polisi mjini Singida akiwaelekeza washitakiwa wanne wa kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha kuingia kwenye gari tayari kwenda kuanza kutumikia adhabu zao kila mmoja miaka 30 jela baada ya kutiwa hatia kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha.Washitakiwa hao walitiwa hatiani kwa kosa la kuteka gari la chuo kikuu cha SUA SU 37012 na kisha kuwapora abiria shilingi 8.7 milioni.Pia walibomoa na kusachi  jeneza lililokuwa limehifadhiwa mwili wa marehemu mwanafunzi wa SUA,Munchari Lyoba uliokuwa ukipelekwa mkoa wa Mara kwa mazishi. 
Mshitakiwa aliyetiwa hatiani kwa kosa la unyang’anyi wa kutimia silaha na kupora abiria wa gari la SUA shilingi 8.7 milioni Hamisi Issah (wa kwanza kulia) akipanda gari tayari kwenda kuanza kutumikia adhabu yake jela miaka 30.Pia mwenye kofia ya bakharasia,Abubakari Jumanne naye katiwa hatiani kwa kosa la unyang’anyi.

Washitakiwa wanne waliotiwa hatiani kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha wakiwa kwenye gari la polisi tayari kwenda kuanza adahabu zao za kila moja miaka 30.Washitakiwa hao walitiwa hatiani kwa kosa la kuteka gari la chuo kikuu cha SUA na kupora abiria shilingi 8.7 milioni.Washitakiwa hao pia inadaiwa walibomoa jeneza lililokuwa limebeba mwili wa mwanafunzi wa SUA Munchari Lyoba na kulisachi kwa imani kuwa limetumika kuhifadhi mali.

Mahakama  ya wilaya ya Singida imewahukumu vijana wakulima wanne wakazi wa Manispaa ya Singida adhabu ya kutumikia jumla ya miaka 120 jela baada ya kupatikana na hatia ya unyang’anyi wa shilingi 8.7 milioni kwa kutumia silaha.

Washitakiwa hao kabla na baada ya unyang’anyi huo walitumia silaha aina ya bunduki,nondo,mawe na fimbo katika kufanikisha azma yao hiyo.

 Washitakiwa hao vijana ambao kila mmoja atatumikia jela miaka 30,ni Hamisi Ally (23),Hamisi Issa (33),Khalid Hamisi (21) na Abubakari Jumanne (26) wote wakazi wa kijiji cha Kisaki Manispaa ya Singida.

Mshitakiwa  aliyekuwa wa kwanza kwenye kesi hiyo Idd Omari (38) mkazi wa kijiji cha Kisaki aliachiwa huru awali baada ya kutokutambuliwa na walalamikaji katika paredi mbili za utambuzi  zilizofanywa na Jeshi la Polisi.

 Washitakiwa hao pia wanadaiwa kuwa baada ya kufanikiwa kupora mali na fedha taslimu waliweza kubomoa jeneza lililokuwa lina mwili wa mwanafunzi wa SUA, Munchari Lyoba na kuchana chana sada kwa imani kwamba kuna mali iliyokuwa imehifadhiwa humo Mwili wa Lyoba alikuwa ukipelekwa Tarime mkoani Mara kuzikwa.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo,Mwendesha Mashitaka Sajenti wa Polisi,Godwel Lawrence amesema pamoja na washitakiwa wote kutokuwa na rekodi yoyote ya makosa ya jinai lakini kitendo walichokifanya ni cha kinyama na cha aibu mbele ya macho ya jamii.

 “Kwa hiyo,Mheshimiwa hakimu naiomba mahakama yako tukufu iwape washitakiwa wote adhabu kali ambayo itakuwa fundisho kwao na watu wengine wanaotarajiwa kufanya makosa ya jinai kwa kutumia silaha au nguvu ya aina yoyote”,amesema Lawrence.

Kwa upande wao washitakiwa kila mmoja kwa nafasi yake walitoa maombolezo yaliyofafana kwamba wana familia zinazowatengea kwa asilimia kubwa na kwamba kosa hilo ni la kwanza kutenda toka wazaliwe Hivyo wakaiomba mahakama hiyo iwape adhabu nafuu.

 Akisoma hukumu hiyo iliyochukua  saa moja na dakika 45,Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Singida,Flora Ndale amesema ushahidi wa upande wa mashitaka umethibitisha bila kuacha chembe chembe ya shaka kwamba washitakiwa wana hatia kama walivyoshitakiwa.

 “Walalamikaji wote ambao walikuwa abiria kwenye gari lililokuwa likisafirisaha mwili wa marehemu mwanafunzi wa SUA maelezo yao yanafafana wote waliweza kuwatambua vema washitakiwa kwa msaada wa taa za gari na mbalamwezi”,amesema.

Ndale amesema kiongozi wa msafara huo Makaranga Nona,aliiambia mahakama kwamba mshitakiwa wa pili na wa tatu walimwamuru kufungua ‘brief case’ mbele ya gari huku mwanga wa taa za gari ukiwamulika.

 “Kama hiyo haitoshi,dereva wa gari hilo Kalistus Malipula ameiambia mahakama hii kwamba

WALIOSACHI MAITI NA KUPORA ZAIDI YA MILLION 19 KORTINI KWA HUKUMU.

 Gari aina ya Land cruiser mali ya chuo cha SUA cha mjini Morogoro kama linavyoonekana baada ya kupigwa mawe na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi  nje kidogo ya mji wa Singida.
 Kesi inayowakabili washitakiwa watano walioteka gari la chuo cha SUA mjini Morogoro na kunyang’anya zaidi ya shilingi 19.8 milioni, hukumu yake inatarajiwa kutolewa kesho na mahakama ya wilaya ya Singida. Utekaji huo ulifanyika Desemba sita mwaka jana saa saba na nusu usiku kwenye barabara kuu ya Dodoma – Singida eneo la Kisaki manispaa ya Singida.
Hudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa mjini Singida ambaye jina lake halikuweza kutambuliwa mara moja,akiliweka sawa baada ya kufanyiwa ukarabati baada ya kubomolewa na majambazi na kulisachi.

KESI inayowakabili washitakiwa watano ya utekaji wa gari la chuo cha SUA Morogoro mjini na kisha kunyang’anya zaidi ya shilingi 19.8 milioni hukumu yake inatarajiwa kutolewa kesho na Mahakama ya Wilaya ya Singida.

Hukumu hiyo inayovutia hisia za wakazi wengi wa Manispaa ya Singida na vitongoji vyake inatarajiwa kusomwa na hakimu wa Wilaya ya Singida Flora Ndale.

Washitakliwa hao inadaiwa baada ya kufanikiwa azma yao ya unyang’anyi wa kutumia silaha za jadi waliweza kufungua jeneza lililokuwa linasafirisha mwili wa mwanafunzi wa SUA Munchari Lyoba na kulisachi kwa imani kwamba kuliwekwa mali.

Washitakiwa hao vijana ni Idd Omari (37),Khalid Hamisi (20), Abubakari Jumanne (25) wote wakazi wa kijiji cha Kisaki Manispaa ya Singida Wengine ni Hamisi Issa (32) mkazi wa kijiji cha Unyamikumbi na Amosi Ally (22) mkazi wa kijiji cha Mtakuja.

Washitakiwa hao wanatuhumiwa kuteka gari linalomilikiwa na SUA lenye namba za usajili SU 37012 ambalo siku ya tukio lilikuwa linaendeshwa na Kalistus Malipula.

Washitakiwa hao waliteka gari hilo desemba sita mwaka jana saa saba na nusu eneo la kijiji cha Kisaki Gari hilo lilikuwa linasafirisha mwili wa mwanafunzi Lyoba kwenda kuzikwa mkoani Mara.


Inadaiwa washitakiwa hao walitumia silaha za jadi ikiwemo
fimbo na mawe kufanikisha azma yao hiyo Waliweka mawe makubwa barabarani kwa lengo la kuzuia magari kupita.

Wednesday, October 23, 2013

FAHAMU SABABU ZINAZOCHANGIA BENKI YA NMB KUWA NA FOLENI NDEFU KULIKO BENKI ZINGINE.

 Meneja wa NMB kanda ya kati, Gabriel Ole Loibanguti akitoa nasaha zake kwenye simena iliyohudhuriwa na wananchama wa klabu ya wafanyabiashara wateja wa NMB.
 Katibu wa klabu ya wanachama wafanyabiashara wa benki ya NMB tawi la Singida,Welu Daniel akitoa nasaha zake kwenye semina ya wananchama hao siku moja iliyofanyika kwenye ukumbi wa Aque Vitae mjini Singida.
 Mwezeshaji wa semina ya siku moja iliyohudhuriwa na wanachama wa klabu ya wafanyabiasha wateja  wa NMB tawi la Singida, Meneja mikopo makao makuu ya NMB jijini Dar-es-salaam,Prisca Pius akitoa mada zake mbalimbali.
 Baadhi ya wananchama wa klabu ya wafanyabiashara wateja wa NMB tawi la Singida waliohudhuria semina ya siku moja iliyohusu kukumbushwa juu ya haki zao kama wateja.
 Baadhi ya viongozi wa NMB waliohudhuria semina ya siku moja ya wananchama wa klabu ya wafanyabiashara wa NMB tawi la Singida.

Meneja wa NMB benki kanda ya kata,Gabriel Ole Loibanguti amewahimiza wateja kujenga utamaduni wa kutoa mapendekezo,maoni na ushauri juu ya uendeshaji wa huduma mbalimbali,ili ziweze kuboreshwa zaidi ziweze kukidhi mahitaji yao.

Loibanguti ametoa wito huo wakati akizungumza kwenye semina ya siku moja iliyohudhuriwa na wananchama wa klabu ya wafanyabiashara wa tawi la NMB Singida. Semina hiyo ilifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Aque Vitae mjini Singida.

Amesema huduma bora zinazotolewa na NMB ambazo zimechangia kwa kiasi kikubwa wateja wengi kuikimbilia benki hiyo,ubora huo umechangiwa na maoni,mapendekezo na ushauri uliotolewa na wateja.

“Kwa hiyo, mimi nisisitize tu kwamba msichoke kutoa maoni,mapendekezo na ushauri wenu juu ya uboreshaji wa huduma zetu.Niwahakikishie kuwa tunajali na kuyafanyia kazi maoni,mapendekezo na ushauri wenu”,amesema meneja huyo wa kanda.

Aidha,Loibanguti alitumia fursa hiyo kuwashauri viongozi wa vilabu vya wananchama wafanyabiashara wa NMB kutembeleana baina ya vilabu ili pamoja na mambo mengine kubadilishana uzoefu kwa manufaa ya ustawi wa NMB.

Kwa upande wake mwezeshaji wa semina hiyo meneja wa masoko kutoka makao makuu ya NMB jijini Dar-es-salaam, Prisca Pius amesema foleni ndefu zilizopo kwenye matawi ya NMB nchini,zinachangiwa na

AUAWA NA KUFUKIWA KWENYE SHIMO LA KINA KIFUPI,FISI WAMFUKUA NA KUMBAKIZA MIFUPA.

Jeshi la Polisi Mkoani Singida limefanikiwa kupata mabaki ya mifupa ya mtu anayedhaniwa kuwa ni Saidi Ngereza (35) mkazi wa Dominiki wilaya ya Mkalama.

Inadaiwa Septemba 30 mwaka huu saa 2.30 usiku Saidi alimuaga mke wake Aziza Khamisi (22) kuwa anakwenda kwa jirani yake kwa ajili ya kumjulia hali kwa vile alikuwa akiumwa.

Habari zaidi zinadai kuwa toka siku hiyo aliyoaga hakurudi nyumbani kwake hadi oktoba 14 mwaka huu saa 6.00 mchana makaki ya mifupa yake yalipogunduliwa hatua kilomita tatu toka nyumbani kwake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Geofrey Kamwela amesema mke wa Saidi, Aziza,aliweza kutambua kuwa mabaki ya mifupa hiyo ni ya mume wake kutokana na nguo zilizokutwa karibu na mabaki ya mifupa hiyo.

“Aziza alitambua nguo hizo ambazo ni suruali ya jeans na bukta nyeusi alizovaa mume wake siku ya Septemba 30 wakati anaaga kwenda kwa jirani kumjulia hali”,alifafanua Kamwela.

Aidha amesema baada ya mabaki ya mifupa hiyo kufanyiwa uchunguzi na daktari ilionekana kuwa

Tuesday, October 22, 2013

Watoto waninginizwa kichwa chini miguu juu huku wakila bakora za nguvu baada ya kulamba sukari.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP Geofrey Kamwela akitoa taarifa ya kushikiliwa kwa mkazi wa kijiji cha Mgongo wilaya ya Iramba Joyce Isaya (30) kwa tuhuma ya kuwafanyia ukatili wa hali ya juu watoto wa kambo kwa madia ya kulamba sukari na kukomba mboga aina ya Mlenda. Mtuhumiwa anadaiwa kuwaning’iniza kwa kamba ya katani kwenye dari watoto hao miguu juu na vichwa chini na kisha kuanza kuwachapa viboko sehemu mbalimbali za miili yao.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida linamshikilia Joyce Isaya (30) mkazi wa kijiji cha Mgongo tarafa ya Shelui wilaya ya Iramba kwa tuhuma ya kuwafanyia ukatili wa hali ya juu watoto wawili.

Mtuhumiwa huyo inadaiwa kuwafunga kamba ya katani miguuni na kuwaning’iniza kwenye dari miguu juu vichwa chini na kuwachapa viboko katika sehemu mbalimbali za miili yao.

Watoto hao ambao ni wa kambo (majina yao tunayo),mmoja ana umri wa miaka 10 na mwingine 8. Inadaiwa kupewa adhabu hiyo kwa madai kuwa walilamba sukari na kukomba mboga yoye aina ya mlenda.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida,ACP,Geofrey Kamwela, amesema tukio hilo la kusikitisha na la ukatili wa hali ya juu,limetokea oktoba 16 mwaka huu saa 9.30 alasiri huko katika kijiji cha Mgongo.

Akifafanua,amesema siku ya tukio majirani walisikia vilio vikali kutoka kwa watoto hao ambao walikuwa wamefungiwa kwenye chumba cha nyumba yao na mama yao wa kambo huku wakichapwa viboko.

“Baada ya majirani hao kufanya uchunguzi ndipo walipowaona watoto hao wamening’inia kwenye dari miguu juu vichwa chini na mama yao huyo wa kambo akiendelea kuwachapa viboko kwenye miili yao.

Baada ya kuona kitendo hicho cha kikatili, majirani hao haraka

Monday, October 21, 2013

WANANCHI WATAKIWA KUWAPA FURSA VIJANA YA MAWAZO KATIKA KAZI



      PICHA ZOTE TOKA MAKTABA YA WWW.SINGIDAYETU.BLOGSPOT.COM

Wananchi mkoani Singida wametakiwa kuwaheshimu vijana wanaofanya kazi katika sekta mbalimbali bila kujali umri wao ili wanufaike na matunda ya kazi hizo.

Afisa ustawi wa jamii mkoa wa Singida Bw Amosi Makala baada ya kugundua  kuwa baadhi ya wananchi hawafiki  katika ofisi za ustawi wa jamii kupata ushauri nasaha pindi wanapokuwa na tatizo.

Bw  Makala amesema baadhi ya watu kama vile wazee  hudharau ushauri wanaopewa na wafanyakazi vijana katika ofisi za ustawi wa jamii kwa kuangalia umri na umbo, jambo ambalo ni hatari katika utendaji kazi na linalokwamisha maendeleo mkoani Singida.

Amesema, ni vyema wananchi kufahamu kuwa endapo hawatafuata ushauri wanaopewa na ustawi wa jamii au kuogopa kufika ofisi hizo wanapokumbana na matatizo mbalimbali kutachangia

AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MIWILI JELA KWA WIZI WA MIFUGO


Mkazi wa  Mwasauya  mkoani Singida amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela baada ya kubainika kutenda kosa wizi wa mifugo.

Akisoma hukumu hiyo hakimu wa mahakama ya mwanzo utemini Joyce Shilla amemtaja mtuhumiwa kuwa ni Msunga Sima kuwa alitenda kosa hilo september 28 mwaka huu.

Hakimu Shilla amesema mshitakiwa akiwa na mwenzake aliyefahamika kwa jina la Rajabu Sidadi waliiba mbuzi wawili na kisha kumchinja mmoja kabla ya

Sunday, October 20, 2013

FAMILIA YANUSURIKA KIFO BAADA YA KIMBUNGA KUEZUA NYUMBA MKOANI SINGIDA




Familia moja imenusurika kufa kufuatia kimbunga kuezua nyumba wanamoishi ,katika wilaya ya ikungi mkoani singida. Tukio hilo limetokea jana majira ya saa kumi na nusu jioni, katika kijiji cha choda kata ya mkiwa tarafa ya Ikungi.

Akizungumza na Singidayetu.blogspot.com diawani wa kata ya mkiwa Bw. Mathias Sungita, ametaja walionusurika kuwa ni familia ya  Bw Saimon Joram.

Imelezwa kuwa upepo mkali uliofuatana na kimbunga ulizingira nyumba ya Bw Sungita, na

MTU MMOJA AFARIKI DUNIA NA WENGINE WAWILI KUJERUHIWA MKOANI SINGIDA



Mtu mmoja amefariki baada ya kupigwa risasi kifuani na mwingine kujeruhiwa mikono yote miwili baada ya watu wasiojulikana kuwavamia na kutaka kuwapora mali katika wilaya ya manyoni mkoani Singida.

Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Igwamadete kata ya iseke tarafa ya Nkonko wilayani manyoni baada ya mtu aliyejulikana kwa jina la Alody Joshua mwenye umri wa miaka 29 kupigwa risasi na majambazi hao
Aidha Daudi Azaliwa amejeruhiwa mikono yote miwili baada ya kupigwa risasi na majambazi hao wakati wakitoka kwenye mnada wa Mpapa kuelekea nyumbani ndipo majambazi hao walipoanza kuwapiga na kuwanyanganya  fedha na kusababisha  kifo cha mtu huyo.

Jeshi la polisi wilayani manyoni limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kufafanua kuwa watu watatu

Friday, October 18, 2013

SINGIDA YAAGIZA DOZI MPYA CHANJO YA UGONJWA WA KIDERI.

 Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida Yahaya Nawanda akizungumza na mwandishi wa habari wa Singida Yetu Blog (hayupo kwenye picha) juu ya kuagizwa kwa njacho mpya ya ugonjwa wa kideri.

Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoa wa Singida Yahaya Nawanda akilisha baadhi ya kuku wake wa kienyeji kati ya 966 anaowafuga kibiashara, katika eneo la nyumba anayoishi.

WILAYA ya Iramba mkoani Singida imelazimika kuagiza  zaidi ya dozi  laki nne za chanjo ya ugonjwa  wa kideri moja kwa moja toka kiwandani, kwa ajili ya kusambaza  kwa wafugaji wa kuku.
Uamuzi huo umefikiwa baada ya kubainika kuwa dawa na chanjo nyingi zinazonunuliwa na   wananchi kwenye maduka binafsi ya kilimo na mifugo zinakuwa zimechakachuliwa na kusababisha kuku kufa.
Akizungumza kwenye  mafunzo ya ufugaji  bora wa kuku, Mkuu wa Wilaya  hiyo Yahaya Nawanda amesema baada ya kubaini tatizo katika chanjo hizo, wameona  vyema kuagiza moja kwa moja toka  kiwandani zinakotengenezwa na kuzimbaza kwa wananchi  wanaofuga kuku Vijijini.
Bwana Nawanda amesema  tayari  mpango huo umeanza kutekelezwa  na  dozi hizo za chanjo zaidi ya laki nne zinatarajiwa kuwa zimewasili  katika Wilaya ya Iramba kabla  ya