Friday, October 18, 2013

SINGIDA YAAGIZA DOZI MPYA CHANJO YA UGONJWA WA KIDERI.

 Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida Yahaya Nawanda akizungumza na mwandishi wa habari wa Singida Yetu Blog (hayupo kwenye picha) juu ya kuagizwa kwa njacho mpya ya ugonjwa wa kideri.

Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoa wa Singida Yahaya Nawanda akilisha baadhi ya kuku wake wa kienyeji kati ya 966 anaowafuga kibiashara, katika eneo la nyumba anayoishi.

WILAYA ya Iramba mkoani Singida imelazimika kuagiza  zaidi ya dozi  laki nne za chanjo ya ugonjwa  wa kideri moja kwa moja toka kiwandani, kwa ajili ya kusambaza  kwa wafugaji wa kuku.
Uamuzi huo umefikiwa baada ya kubainika kuwa dawa na chanjo nyingi zinazonunuliwa na   wananchi kwenye maduka binafsi ya kilimo na mifugo zinakuwa zimechakachuliwa na kusababisha kuku kufa.
Akizungumza kwenye  mafunzo ya ufugaji  bora wa kuku, Mkuu wa Wilaya  hiyo Yahaya Nawanda amesema baada ya kubaini tatizo katika chanjo hizo, wameona  vyema kuagiza moja kwa moja toka  kiwandani zinakotengenezwa na kuzimbaza kwa wananchi  wanaofuga kuku Vijijini.
Bwana Nawanda amesema  tayari  mpango huo umeanza kutekelezwa  na  dozi hizo za chanjo zaidi ya laki nne zinatarajiwa kuwa zimewasili  katika Wilaya ya Iramba kabla  ya
mwisho wa mwezi huu.

Ufugaji wa kuku wa asili ni moja shughuli kuu za kiuchumi kwa wananchi wa mkoa wa Singida ambapo inakadriwa kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana zaidi ya kuu milioni mbili walikuwa wanafugwa.

No comments:

Post a Comment