Sunday, January 27, 2013

WAANGUKA NA UNGO KATIKA KITUO CHA POLISI MANYONI


Jeshi la polisi wilaya ya Monyoni mkoani Singida linawashikilia vijana watatu waliokuwa wakisafiri kwa kutumia ungo kutoka katika kijiji cha

Saturday, January 26, 2013

Mkoa wa Singida wazindua mradi wa pikipiki kwa ajili ya kudhibiti uhalifu

 Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Vicent Kone (mwenye suti nyeusi) akisalimiana na baadhi ya  viongozi wa jeshi polisi mkoa wa Singida muda mfupi kabla ya kuzindua mradi wa pikipiki kwa ajili ya wakaguzi wa tarafa mkoani Singida.
 Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Vicent Kone akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi wa pikipki kwa ajili ya ukaguzi wa makosa ya uhalifu katika tarafa za mkoa wa Singida. Kushoto ni Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida Linus Sinzumwa na kushoto ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida,Mgana Msindai.
 Baadhi ya askari wa jeshi la polisi mkoa wa Singida wakishuhudia uzinduzi wa mradi wa pikipiki kwa ajili ya ukaguzi wa makosa ya uhalifu katika tarafa za mkoa wa Singida.
 Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Vicent Kone akijaribu kuendesha pikipiki za mradi wa ukaguzi wa makosa ya uhalifu katika tarafa za mkoa wa Singida. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singid Mgana Msindai akishuhudia tukio hilo.
Baadhi ya pikipiki 22 za mradi wa ukaguzi wa makosa ya uhalifu katika tarafa za mkoa wa Singida. Pikipiki hizo zimetolewa rasmi kwa ajili ya kukabidhiwa maafisa polisi wa tarafa za mkoa wa Singida.

Wanafunzi mkoani Singida watakiwa kujenga utamaduni wa kupanda miti katika makazi yao

 Mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Kone akishiriki kupanda miti katika siku ya uzinduzi wa miti ki-mkoa.Uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya shule ya sekondari ya Unyamikumbi manispaa ya Singida.
 Naibu meya wa manispaa ya Singida, Shaban Mkata akishiriki kupanda mti kwenye uzinduzi wa upandaji miti ki mkoa uliofanyika katika shule ya sekondari ya Unyamikumbi manispaa ya Singida.

Diwani wa viti maalum Mama Alute akipanda mti kwenye uzinduzi wa upandaji miti kimkoa.
 Baadhi ya wakazi wa kata ya Kisaki manispaa ya Singida na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Unyamikumbi wakimsikiliza kwa makini mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone (hayupo kwenye picha) akizungumza kwenye hafla ya upandaji miti ki-mkoa.

Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone amewaagiza wanafunzi kujenga utamaduni wa kupanda miti miwili katika makazi yao kila mwaka na kuitunza na kuilinda vizuri ili iweze kukua.
 Dkt.Kone ametoa wito huo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa upandaji miti ki-mkoa,uliofanyika katika viwanja vya shule ya sekondari ya kata ya Unyamikumbi manispaa ya Singida.
 Amesema kijana akijenga utamaduni wa kupanda miti na kuitunza vizuri, kwanza atakuwa

Friday, January 25, 2013

Mbunge wa Singida mjini atoa msaada wa vitenge vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 60 ili kufanikisha maadhimisho ya miaka 36 ya CCM

 Katibu wa CCM manispaa ya Singida Mkude (kushoto) akikabidhiwa moja ya pea 7,500 za vitenge na msaidizi wa mbunge wa jimbo la Singida mjini Duda Mughenyi (kulia). Vitenge hivyo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 60,vimetolewa msaada na mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji, kwa ajili ya kufanikisha maandalizi ya sherehe ya CCM kutimiza miaka 36.
 Mwenyekiti wa CCM manispaa ya Singida Hamisi Nguli (kulia) akikabidhiwa pea ya kitenge na katibu uchumi na fedha wa CCM manispaa ya Singida.
 Msaidizi wa mbunge wa jimbo la Singida mjini Duda Mughenyi (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa CCM manispaa ya Singida, waliohudhuria makabidhiano ya pea 7,500 zilizotolewa na mbunge wa Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji, kwa ajili ya sherehe za CCM kutimiza miaka 36.
 Baadhi ya mabeli ya vitenge pea 7,500 vilivyotolewa na mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji kufanikisha maandalizi ya sherehe za CCM kutimiza miaka 36.
Baadhi ya wanavikundi vya uhamasishaji vya CCM  na viongozi wa CCM manispaa ya Singida, waliohudhuria makabidhiano ya vitenge vilivyotolewa msaada na mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji, kwa ajili ya kufanikisha maandalizi ya sherehe za CCM kutimiza miaka 36.
 
Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji ametoa msaada wa pea za vitenge 7,500 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 60, kwa ajili ya kufanikisha maandalizi ya sherehe za CCM kutimiza miaka 36 toka kianzishwe.
Mh. Dewji ametoa msaada huo mkubwa na wa aina yake, baada ya kuombwa kufanya hivyo na

Tuesday, January 22, 2013

CCM Manispaa ya Singida yawataka vijana kuwa makini sana na maandamano yasio na faida kwao

Mwenyekiti wa CCM manispaa ya Singida Hamisi Nguli akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo vilivyotolewa msaada na mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh.Mohammed Gullam Dewji.

Vijana katika halmashauri ya manispaa ya Singida wameshauriwa kufanya utafiti wa kina juu ya faida na hasara ya ushiriki wa maandamano yanayoitishwa na watu au viongozi mbalimbali wakiwemo wa siasa, kabla ya kushiriki.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa CCM manispaa ya Singida Hamisi Nguli wakati akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 31.9 ilivyotolewa bure na mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji.
Ameisema kwa kawaida, kijana yeyote huwa

Mkuu wa wilaya ya Singida ahimiza upandaji Miti kijiji cha Ilongero

 Mkuu wa wilaya ya Singida Mwalimu Queen Mlozi akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa kilele cha upandaji miti ki-wilaya uliofanyika kwenye kijiji cha Ilongero.
 Mkuu wa wilaya ya Singida Mwalimu Queen Mlozi akishiriki kutoa burudani na kikundi cha uhamsishaji cha kijiji cha Ilongero wakati wa upandaji miti ki-wilaya uliofanyika katika kijiji cha Ilongero.
Mzee Athumani Sungi (71) akifurahia kitendo cha mjukuu wake kumsaidia kupanda mti katika chanzo cha maji kijiji cha Ilongero jimbo la Singida kaskazini.

Monday, January 21, 2013

Katibu tawala mkoa wa Singida aitaka PSPF kuangalia uwezekano wa kuanza kutoa malipo ya kiinua mgongo katika muda wa siku mbili.

 Katibu tawala mkoa wa Singida Liana Hassan akifungua semina ya simu moja ya wadau wa mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umma (PSPF) mkoa wa Singida. Semina hiyo ilihudhuriwa na wadau mbali mbali wa PSPF  na lengo ilikuwa kuhamasisha watumishi wa umma wengi zaidi wanajiunga na mfuko huo.Kushoto ni afisa mfawidhi wa PSPF mkoa wa Singida Said Majimoto na kulia ni afisa mwingine wa PSPF Erick Mafuru.
 Afisa mfuko wa PSPF mkoa wa Singida Erick Mafuru akitoa mada yake kwenye semina ya siku moja ya wadau mbalimbali wa mfuko huo (hawapo kwenye picha) mkoani Singida.
Baadhi ya wadau wa mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umma (PSPF) waliohudhuria semina ya siku moja iliyoandaliwa na mfuko huo mkoani Singida.

Mfuko wa wa pensheni kwa watumishi wa umma (PSPF) mkoa wa Singida umeshauriwa kuongeza juhudi katika kujitangaza na kuwa wabunifu ili uweze kuwavutia waajiriwa na kuongeza wanachama wengi zaidi.
Katibu tawala mkoa wa Singida Liana Hassan ametoa changamoto hiyo wakati akifungua semina ya siku moja ya wadau wa mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umma wa mkoa wa Singida.
Amesema  PSPF mkoa wa Singida wanalo jukumu la kuhakikisha mfuko huo wa hifadhi unaendelea kukua, kuwekeza zaidi na kuwa endelevu.
Akifafanua zaidi, Liana amesema uendelevu na kukua kwa mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umma (PSPF), utategemea sana uendelevu wa

Thursday, January 17, 2013

Zaidi ya Million 31.9 zagharamia vifaa ligi ya Mohammed Dewji, Singida.

 Mwenyekiti wa CCM jimbo la Singida mjini, Hamisi Nguli (kushoto) akikabidhi vifaa vya michezo kwa kiongozi wa tawi la  Mitunduruni.
 Foleni ya viongozi wa matawi katika jimbo la Singida mjini wakikabidhiwa vifaa vya michezo kwa ajili ya timu zao kushiriki kombe la MO inayotarajiwa kuanza Januari 20 mwaka huu.
 Baadhi ya wa viongozi ngazi za matawi jimbo la Singida mjini, wakimsikiliza kwa makini mwenyekiti wa CCM manispaa ya Singida, Hamisi Nguli (hayupo kwenye picha) wakati akitoa nasaha zake muda mfupi kabla ya kukabidhi vifaa vya michezo.
Baadhi ya msaada wa vifaa vya michezo vilivyotolewa na mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji kwa ajili ya kuendeleza mchezo wa soka jimboni kwake.

Mbunge wa jimbo la Singida mjini,Mohammed Gullam Dewji,ametoa msaada wa vifaa mbalimbali vya michezo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 31.9 vitakavyotumika kwenye ligi ya kombe lake, inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi

Wednesday, January 16, 2013

Wakazi wa Iramba watakiwa kulinda misitu.

 Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoa wa Singida,Yahaya Nawanda akizungumza kwenye kilele cha siku ya upandaji miti kitaifa wilayani Iramba uliofanyika katika kijiji cha Mbelekese kata ya Ndago.Kushoto (aliyekaa) ni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Iramba,Christina Midelo.
 Mkuu wa wilaya ya Iramba Yahaya Nawanda akishiriki kupanda miti katika siku ya upandaji miti kitaifa iliyofanyika kiwilaya katika kijiji cha Mbelekese.
 Maafisa wa maliasili na utalii kanda ya kati, Muze Kajiru (katikati) mtaalamu wa nyuki na mazingira,William Kaaya (kushoto)mtaalamu wa misitu na mazingira na Zakaria Matavi (kulia) mtaalamu wa misitu wakishiriki kupanda miti katika siku ya kupanda miti ya wilaya ya Iramba.
Mkuu wa wilaya ya Iramba Yahaya Nawanda (wa tano kutoka kushoto) akipokea miche ya miti mbalimbali elfu moja  iliyotolewa na ofisi ya malialisi na utalii kanda ya kati.Nawanda alikabidhiwa na Muze Kajiru mtaalamu wa nyuki na mazinmgira kanda ya kati.

Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Yahaya Nawanda ameagiza kila mkazi wa wilaya hiyo kuwa mlinzi wa misitu ili kulinda maliasli hiyo ambayo ni uhai wa viumbe vyote hai inayokabiliwa na tishio la kutoweka.
Nawanda aliyasema hayo jana wakati akizungumza kwenye kilele cha siku ya  upandaji miti wilayani humo  uliofanyika kwenye kijiji cha Mbelekese kata ya Ndago jimbo la Iramba magharibi.
Alisema uvunaji ovyo wa miti katika wilaya hiyo,umesababisha madhara mengi ikiwemo ukame mkali,uhaba wa mvua na

Wazee wa CCM Singida Wateta na Mangula Dar.

 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula (kushoto) akiwasikiliza Wazee waasisi wa CCM kutoka mkoani Singida, Kutoka kushoto, Sumbu Galawa, Alhaji Mahami Rajabu Kundya na  Mujengi Gwao Makamu, walipomfikishia ujumbe wao maalum, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam
 Mzee Sumbu Galawa akimkabidhi ujumbe maalum, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pilip Mangula, wakati yeye Wazee wenzake wa CCM kutoka mkoani Singida, Alhaji Rajabu Kundya (wapili kulia) na Mujengi Gwao (watatu kulia) walipofika Ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam,kuwasilisha ujumbe huo.
  Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Phili Mangula akimshukuru Mzee Sumbu Galawa, baada ya kupokea ujumbe uliowasilishwa kwake na Wazee wa CCM kutoka mkoani Singida, Ofisi leo Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam.
Mangula akizungumza na Wazee wa CCM kutoka mkoa wa Singida, waliofika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM,Lumumba Dar es Salaam, kumpa ujumbe maalum wa kuimarisha chama. Kushoto ni Mzee Sumbu Galawa na kulia ni  Alhaj Mahami Rajabu Kundya na  Mujengi Gwao.

Tuesday, January 15, 2013

Ajali za Barabarani Mkoani Singida zapungua kwa asilimia 12 ikilinganishwa na mwaka juzi.

 Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida Linus Sinzumwa akitoa taarifa yake ya utekelezaji kwa kipindi cha mwaka jana kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha). Kulia ni mwenyekiti mstaafu wa klabu ya waandishi wa habari mchungaji Emmanuel Barnaba na kulia ni diwani wa kata ya Mitunduruni,Pantaleo Sorongai.
 Diwani wa kata ya Utemini manispaa ya Singida Baltazar Kimario akizungumza wakati wa ufunguzi wa tafrija iliyoandaliwa na jeshi la polisi mkoa wa Singida kwa ajili ya kutoa taarifa yake ya utekelezaji kwa kipindi cha mwaka jana na pia kupongeza waandishi wa habari kwa ushirikiano wao mzuri kwa jeshi hilo. Wa pili kutoka kulia ni kamanda wa polisi mkoa wa Singida Linus Sinzumwa.Kutoka kushoto ni mkuu wa magereza mkoa wa Singida na anayefuatia ni diwani wa kata ya Mitunduruni manispaa ya Singida Pantaleo Sorogai.
Baadhi ya waandishi wa habari na maofisa wa jeshi la polisi mkoani Singida waliohudhuria hafla iliyoandaliwa na polisi kwa ajili ya kutoa taarifa yake ya utekelezaji kwa kipindi cha mwaka jana na pia kuwapongeza waandishi wa habari kwa ushirikiano wao mzuri na jeshi hilo.

Jeshi la polisi mkoani Singida kitengo cha usalama barabarani, limekusanya tozo (notification) zaidi ya shilingi 487.9 milioni zilizotokana na makosa mbali mbali ya usalama barabarani kwa kipindi cha mwaka jana.
Akitoa taarifa yake ya utekelezaji ya mwaka jana kwa waandishi wa habari, Kamanda wa polisi mkoa wa Singida Linus Sinsumwa amesema kiasi hicho kilichokusanywa, kimeongezeka kwa asilimia 66.2 ikilinganishwa na kiasi cha shilingi

Saturday, January 12, 2013

Mgana Msindai awataka madereva Singida kutii sheria bila shurti kuepukana na usumbufu.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida,Mgana Msindai (mwenye kofia ya tunga) akikabidhiwa zawadi ya mbuzi mbili na viongozi wa umoja wa mabasi madogo (Hiace) mjini Singida.Umoja huo umetoa zawadi hiyo kwa kitendo cha mwenyekiti huyo kufanikisha mabasi madogo yaanze kutumia kituo cha zamani cha mabasi mjini Singida.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Mgana Msindai amewahimiza madereva wa vyombo vya moto yakiwemo mabasi madogo kutii sheria bila shurti, ili kuepuekana na usumbufu unaochangia kupoteza muda mwingi.
Msindai ametoa wito huo wakati akizungumza na viongozi wa umoja wa madereva wa mabasi madogo (hiece) yanayofanya safari kati ya

Wakazi wa Singida wenye maradhi yanayohitaji upasuaji kupatiwa tiba na madaktari bingwa kutoka Marekani.

                                   Jengo la hospitali ya mkoa lililopo Singida mjini.

Madaktari bingwa 26 kutoka Marekani wataendesha zoezi maalumu la utoaji tiba kwa wagonjwa wenye maradhi yanayohitaji upasuaji, utakaofanyika katika hospitali ya mkoa wa Singida.
Akiongea na Singida Yetu Blog, Mganga mfawidhi hospitali ya mkoa Singida Dkt. Suleiman Muttan amesema huduma hiyo ni mpango wa kila mwaka wa Shirika la Outriach International kutoa huduma hiyo Singida.
Dkt. Muttan amesema, kati ya wataalamu mbalimbali wanaokuja, watakuwepo pia madaktari bingwa wa

Manispaa ya Singida yafanikiwa kupanda miti zaidi ya milioni 2.6 katika kipindi cha miaka minne.

 Mkuu wa wilaya ya Singida mwalimu Queen Mlozi,akishiriki kupanda miti katika siku ya uzinduzi wa upandaji miti katika manispaa ya Singida.
Mkuu wa wilaya ya Singida mwalimu Queen Mlozi akizungumza na wananchi waliohudhuria uzinduzi wa  siku ya upandaji miti katika manispaa ya Singida.Uzinduzi huo ulifanyika katika shule ya msingi na Unyinga kata ya Mandewa.

Halmashauri  ya manispaa ya Singida imepanda miti 2,645,314 ya aina mbalimbali katika kipindi cha miaka minne iliyopita.
Akitoa taarifa yake fupi siku ya uzinduzi wa upandaji miti katika manispaa hiyo, Mkurugenzi wa manispaa ya Singida Mathias Mwangu amesema zoezi la upandaji miti katika manispaa hiyo, lengo lake ni kuzuia mmomonyoko wa ardhi na kudhibiti kuenea kwa

Thursday, January 10, 2013

Shule za sekondari Singida zatakiwa kuwa na maabara tatu zilizokamilika kabla ya Novemba 2013.

 Mkuu wa wilaya ya Singida mwalimu Queen Mlozi (wa pili kushoto) akikagua ujenzi wa maabara tatu za shule ya sekondari kata ya Mitunduruni  jimbo la Singida mjini.Wa kwanza kushoto ni diwani wa kata ya Mitunduruni,Sorongai Pantaleo.
 Diwani wa kata ya Mitundurinu (CCM) jimbo la Singida mjini,Sorongai Pantaleo (wa kwanza kushoto) akizungumza na mkuu wa wilaya ya Singida mwalimu Queen Mlozi ofisini kwa mkuu wa shule ya sekondari kata ya Mitunduruni.
 Mkuu wa wilaya ya Singida,mwalimu Queen Mlozi, (wa pili kutoka kulia) akikagua ujenzi wa choo katika shule ya msingi ya Unkyankindi kata ya Mitunduruni.Wa kwanza kulia ni diwani wa kata ya Mitunduruni Bw.Sorongai Pantaleo.
Baadhi ya vyumba vya madarasa  vilivyojengwa na mbunge wa jimbo la Singida mjini,Mohammed Gullam Dewji.
  
Mkuu wa wilaya ya Singida Mwalimu Queen Mlozi amewahimiza wakuu wa shule za sekondari kuwa wabunifu katika kutafuta misaada na fedha kwa ajili ya kugharamia ujenzi  wa maabara.
Amesema kwa vile sio rahisi kwa serikali kufanya kila kitu ikiwemo kujenga kwa mpigo maabara katika shule zote za sekondari nchini, kuna umuhimu mkubwa kwa wananchi na wadau wengine kusaidiana na serikali.
Mkuu huyo wa wilaya ametoa changamoto hiyo wakati akizungumza na

Mkoa wa Singida wafanikiwa kupunguza idadi ya vifo vya kina mama wajawazito na watoto hadi kufikia 85 kwa kila laki moja.

            Sehemu ya hospitali ya rufaa ya mkoa wa Singida inayoendelea kujengwa hivi sasa.

Mkoa wa Singida umetumia zaidi ya shilingi bilioni 6.1 kugharamia ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2009 hadi mwaka jana.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone amebainisha hayo wakati akitoa taarifa yake ya utekelezaji wa

Wakati mwingine na sisi abiria tuna makosa, hebu tazama hii picha ni nani wakulaumiwa ajali inapotokea..?!

 Landrover aina ya 110 T.973 AFO inayosafirisha abiria na mizigo kati ya Singida mjini na kijiji cha Londoni kilichopo wilaya ya Manyoni,ikiwa imesheheni mizigo ikisukumwa tayari kuanza safari ya kwenda Londoni.
Landrover aina ya 110 T.973 AFO ikiwa imesheheni mizigo ya wafanyabishara wa kijiji cha Londoni wilayani Manyoni. Mzigo ukiwa mkubwa kitendo kinachohatarisha maisha ya abiria.