Mkuu wa mkoa wa Singida
Dk.Parseko Kone akishiriki kupanda miti katika siku ya uzinduzi wa miti
ki-mkoa.Uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya shule ya sekondari ya
Unyamikumbi manispaa ya Singida.
Naibu meya wa manispaa ya
Singida, Shaban Mkata akishiriki kupanda mti kwenye uzinduzi wa upandaji
miti ki mkoa uliofanyika katika shule ya sekondari ya Unyamikumbi
manispaa ya Singida.
Diwani wa viti maalum Mama Alute akipanda mti kwenye uzinduzi wa upandaji miti kimkoa.
Baadhi ya wakazi wa kata ya
Kisaki manispaa ya Singida na wanafunzi wa shule ya sekondari ya
Unyamikumbi wakimsikiliza kwa makini mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko
Kone (hayupo kwenye picha) akizungumza kwenye hafla ya upandaji miti
ki-mkoa.
Mkuu
wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone amewaagiza wanafunzi kujenga
utamaduni wa kupanda miti miwili katika makazi yao kila mwaka na
kuitunza na kuilinda vizuri ili iweze kukua.
Dkt.Kone
ametoa wito huo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa upandaji miti
ki-mkoa,uliofanyika katika viwanja vya shule ya sekondari ya kata ya
Unyamikumbi manispaa ya Singida.
Amesema
kijana akijenga utamaduni wa kupanda miti na kuitunza vizuri, kwanza
atakuwa
anaipenda na kuithamini miti na kwa njia hiyo, atahakikisha miti
haivunwi hovyo kitendo kitakachochangia mkoa kutokugeuka jangwa.
Dtk.
Kone amewataka kuwa na utamaduni huo wa kupanda miti miwili moja ukiwa
wa matunda, uendelezwe hadi katika shule na vyuo watakapo bahatika
kupitia.
Amesema
endapo wanafunzi kila mmoja atatekeleza agizo hilo kwa makini, watakuwa
wameshiriki vyema katika mapambano dhidi ya mkoa na nchi kugeuka
jangwa.
No comments:
Post a Comment