Tuesday, January 22, 2013

CCM Manispaa ya Singida yawataka vijana kuwa makini sana na maandamano yasio na faida kwao

Mwenyekiti wa CCM manispaa ya Singida Hamisi Nguli akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo vilivyotolewa msaada na mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh.Mohammed Gullam Dewji.

Vijana katika halmashauri ya manispaa ya Singida wameshauriwa kufanya utafiti wa kina juu ya faida na hasara ya ushiriki wa maandamano yanayoitishwa na watu au viongozi mbalimbali wakiwemo wa siasa, kabla ya kushiriki.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa CCM manispaa ya Singida Hamisi Nguli wakati akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 31.9 ilivyotolewa bure na mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji.
Ameisema kwa kawaida, kijana yeyote huwa
amejawa na matengemeo na matarajio mengi kupindukia akilini mwake na kitendo hicho ni rahisi mno kudanganyika.
Amesema hivi sasa wapinzani wanalielewa hilo na ndio maana wameelekeza nguvu zao zote kwa vijana kuwadanganya kwa vile wanajua ni rahisi kuingia mkenge.
Ameongeza kuwa angalia maandamano y oyote utakuta vijana ni asilimia 99, na ukiwauliza nini kilichowapeleka kuandamana na kuacha kazi za kuwaingizia kipato halali, wanakuwa hawana jibu la maana.
Kwa hali hiyo, Nguli amewataka vijana kuwa makini sana na maandamano kwa madai kuwa yanasababisha hasara nyingi ikiwemo vilema vya kudumu na wakati mwingine vifo.
Nguli amewataka vijana kutulia na kuchapa kazi halali kwa bidii na kujielimisha kwa kadri ya uwezo wao utakavyowaruhusu.

No comments:

Post a Comment