Friday, January 25, 2013

Mbunge wa Singida mjini atoa msaada wa vitenge vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 60 ili kufanikisha maadhimisho ya miaka 36 ya CCM

 Katibu wa CCM manispaa ya Singida Mkude (kushoto) akikabidhiwa moja ya pea 7,500 za vitenge na msaidizi wa mbunge wa jimbo la Singida mjini Duda Mughenyi (kulia). Vitenge hivyo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 60,vimetolewa msaada na mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji, kwa ajili ya kufanikisha maandalizi ya sherehe ya CCM kutimiza miaka 36.
 Mwenyekiti wa CCM manispaa ya Singida Hamisi Nguli (kulia) akikabidhiwa pea ya kitenge na katibu uchumi na fedha wa CCM manispaa ya Singida.
 Msaidizi wa mbunge wa jimbo la Singida mjini Duda Mughenyi (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa CCM manispaa ya Singida, waliohudhuria makabidhiano ya pea 7,500 zilizotolewa na mbunge wa Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji, kwa ajili ya sherehe za CCM kutimiza miaka 36.
 Baadhi ya mabeli ya vitenge pea 7,500 vilivyotolewa na mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji kufanikisha maandalizi ya sherehe za CCM kutimiza miaka 36.
Baadhi ya wanavikundi vya uhamasishaji vya CCM  na viongozi wa CCM manispaa ya Singida, waliohudhuria makabidhiano ya vitenge vilivyotolewa msaada na mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji, kwa ajili ya kufanikisha maandalizi ya sherehe za CCM kutimiza miaka 36.
 
Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji ametoa msaada wa pea za vitenge 7,500 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 60, kwa ajili ya kufanikisha maandalizi ya sherehe za CCM kutimiza miaka 36 toka kianzishwe.
Mh. Dewji ametoa msaada huo mkubwa na wa aina yake, baada ya kuombwa kufanya hivyo na
Katibu wa CCM manispaa ya Singida.
Msaidizi wa mbunge Dewji, Duda Mughenyi, amesema jumla ya vikundi vya uhamasihaji 112, vimenufaika na msaada huo wa vitenge.
Amesema  pamoja na vikundi hivyo, pia wajumbe wa halmashauri kuu ya matawi, wafanyabiashara wa kuku za kienyeji soko kuu, boda boda na taasisi mbali mbali, watanufaika na msaada huo.
Msaidizi huyo wa mbunge, amesema kwa hali hiyo, sherehe hii muhimu, ni lazima nayo ipewe heshima ya aina yake ikiwemo wana- CCM na wapenzi wake, waonekane tofauti siku hiyo ya sherehe.

No comments:

Post a Comment