Monday, January 21, 2013

Katibu tawala mkoa wa Singida aitaka PSPF kuangalia uwezekano wa kuanza kutoa malipo ya kiinua mgongo katika muda wa siku mbili.

 Katibu tawala mkoa wa Singida Liana Hassan akifungua semina ya simu moja ya wadau wa mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umma (PSPF) mkoa wa Singida. Semina hiyo ilihudhuriwa na wadau mbali mbali wa PSPF  na lengo ilikuwa kuhamasisha watumishi wa umma wengi zaidi wanajiunga na mfuko huo.Kushoto ni afisa mfawidhi wa PSPF mkoa wa Singida Said Majimoto na kulia ni afisa mwingine wa PSPF Erick Mafuru.
 Afisa mfuko wa PSPF mkoa wa Singida Erick Mafuru akitoa mada yake kwenye semina ya siku moja ya wadau mbalimbali wa mfuko huo (hawapo kwenye picha) mkoani Singida.
Baadhi ya wadau wa mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umma (PSPF) waliohudhuria semina ya siku moja iliyoandaliwa na mfuko huo mkoani Singida.

Mfuko wa wa pensheni kwa watumishi wa umma (PSPF) mkoa wa Singida umeshauriwa kuongeza juhudi katika kujitangaza na kuwa wabunifu ili uweze kuwavutia waajiriwa na kuongeza wanachama wengi zaidi.
Katibu tawala mkoa wa Singida Liana Hassan ametoa changamoto hiyo wakati akifungua semina ya siku moja ya wadau wa mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umma wa mkoa wa Singida.
Amesema  PSPF mkoa wa Singida wanalo jukumu la kuhakikisha mfuko huo wa hifadhi unaendelea kukua, kuwekeza zaidi na kuwa endelevu.
Akifafanua zaidi, Liana amesema uendelevu na kukua kwa mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umma (PSPF), utategemea sana uendelevu wa
michango na kuongezeka kwa idadi ya wanachama.
Katika hatua nyingine, Katibu tawala huyo ameutaka mfuko huo kuangalia uwezekano wa kuanza kutoa malipo ya kiinua mgongo katika muda wa siku mbili badala ya siku saba za sasa.
Aidha, Liana amesema kwa vile teknolojia imeendelea zaidi, si vibaya kuwe na “mobile”  zaidi kuwezesha mwanachama kuangalia salio au michango yao kupitia huduma ya simu za viganjani po pote walipo.
Awali Afisa Mfawidhi wa PSPF mkoa wa Singida Said Majimoto, alitaja mada za semina hiyo kuwa ni pamoja na PSPF ni nini, nani mwanachama wa PSPF, majukumu ya mfuko, kutambua na kusajili wananchama na ukusanyaji wa michango.
Aidha, Majimoto alitaja mafao yanayotolewa na PSPF – tuzo la wastaafu kuwa ni mafao ya uzeeni, mafao ya ulemavu, mafao ya kifo na msaada wa mazishi.
Kwa mijubu wa afisa huyo,  mapato ya PSPF ni michango ya wananchama ambayo ni asilimia tano ya mshahara wa kila mwezi.
Pia mchango wa mwajiri ambao ni aslimia 15 ya mshahara wa kila mwezi wa mwanachama na faida inayopatikana kutokana na uwekezaji.

No comments:

Post a Comment