Sehemu ya hospitali ya rufaa ya mkoa wa Singida inayoendelea kujengwa hivi sasa.
Mkoa
wa Singida umetumia zaidi ya shilingi bilioni 6.1 kugharamia ujenzi wa
hospitali ya rufaa ya mkoa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2009 hadi
mwaka jana.
Mkuu
wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone amebainisha hayo wakati akitoa
taarifa yake ya utekelezaji wa
ilani ya uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha
mwaka 2005 hadi mwaka jana.
Amesema
fedha hizo zimetumika kugharamia ujenzi wa majengo mawili ya wagonjwa
wa nje (OPD) na jengo la wazazi ambayo tayari yamekamilika.
Dkt.
Kone amesema pia fedha hizo zimetumika katika ujenzi wa awamu ya pili
ya mradi huo kwa kujenga jengo la utambuzi wa magonjwa ambalo
limekamilika kwa asilimia 95.
Amesema
kwa mwaka huu wa fedha wa 2012/2013, serikali kuu imewatengea shilingi
bilioni 1,805,154,000 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa hospitali ya
rufaa.
Kuhusu
vifo vya akina mama wajawazito, mkuu huyo amesema vifo hivyo
vinavyotokana na uzazi, vimepungua kutoka 233/100,000 vya mwaka 2005,
hadi vifo 87/100,000 kwa kila vizazi hai juu mwaka jana.
Mkuu
huyo wa mko amesema mafanikio hayo yametokana na kuongezeka kwa idadi
ya akina mama wajawazito kujifungulia katika vituo vya afya.
No comments:
Post a Comment