Saturday, January 5, 2013

Mgana Msindai awataka wana CCM Singida kufanya kazi halali ili kujiletea maendeleo.

 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, Mgana Izumbe Msindai akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kituo cha zamani cha mabasi mjini Singida, Msindai alikuwa akijitambulisha kuvunja makundi na kupokea kero mbalimbali za wananchi.
Baadhi ya wanaccm na wananchi wa Singida mjini wakimsikiliza kwa makini mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, Mgana Izumbe Msindai (hayupo kwenye picha) wakati akihutubia.

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi  wa mkoa wa Singida kwa ujumla,  wameaswa kutumia mwaka  huu mpya,  kujiwekea malengo  ya kufanya kazi  halali kwa bidii  na maarifa  ili waweze kujiletea maendeleo  makubwa zaidi kuliko
yaliyopatikana mwaka jana.
Changamoto hiyo imetolewa  na Mwenyekiti wa CCM Mkoa Singida Mgana Izumbe Msindai, wakati akiutubia wananchi  wa Manispaa  ya Singida kwenye kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kituo kikuu cha mabasi cha zamani mjiniSingida.
Amesema  kujituma  kufanya kazi kwa bidii, maarifa  na kwa malengo,  ndio njia pekee inayoweza kumsaidia mwananchi ye yote kujikomboa kiuchumi na kupelekea  kuishi maisha bora.
Akifafanua zaidi, Msindai amesema linapokuja suala la maendeleo, ni lazima itikadi za kisiasa ziwekwe pembeni, ili maendeleo endelevu ya mtu mmoja mmoja, wilaya, mkoa na hata taifa, yaweze kupatikana.
Msindai  ambaye ni maarufu kwa jina la CRDB benki inayomjali mteja, ametumia fursa hiyo kuwashukuru wana CCM kwa kumchagua kwa kishindo kushika nafasi ya mwenyekiti CCM Mkoa.
Wakati huo huo, Msindai amesema kuwa wamekubaliana na manispaa ya Singida, kituo kikuu cha zamani cha mabasi, kuanzia sasa kitumike kwa mabasi madogo kushusha abiria hadi hapo manispaa itakapoanza kujenga kitega uchumi.

No comments:

Post a Comment