Friday, January 4, 2013

Mkuu wa wilaya ya Singida ahimiza watoto kupelekwa kupata chanjo za Rotarix na PCV 13.


  Mkuu wa wilaya ya Singida,mwalimu Queen Mlozi (katikati) akitoa chanjo ya Rotarix kwa mtoto muda mfupi baada ya kuzindua utoaji wa chanjo hizo.
Baadhi ya watoto wakiwa wanasubiri kupata chanjo mpya za Rotarix inayokinga ugonjwa wa kuharisha na PCV inayokinga ugonjwa wa Nimonia.Uzinduzi wa chanjo hizo ulifanyika katika kituo cha afya cha Sokoine mjini Singida kwa ngazi ya wilaya ya Singida.

Serikali wilayani Singida imewahimiza viongozi  na watendaji wote serikalini, vyama vya siasa, dini, taasisi na wadau wote, kushiriki kikamilifu kuhakikisha jamii inapata taarifa sahihi kuhusu chanjo mbili mpya za
Rotarix na PCV 13.
Chanjo ya Rotarix, inakinga ugonjwa wa kuharisha na PCV 13 inakinga ugonjwa wa nimonia kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa wilaya hiyo Mwalimu Queen Mlozi wakati akizindua chanjo hizo mpya kwenye kituo cha afya cha Sokoine mjini Singida.
Amesema utafiti uliofanywa juu ya vifo vya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano, imebainika magonjwa ya kuharisha na nimonia yana mchango mkubwa katika vifo hivyo.
Mlozi amesema kutokana na utafiti huo, serikali imeamua kuanzisha chanjo hizo mpya ili kudhibiti vifo hivyo vinavyotokana na kuharisha na nimonia.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘mtoto asiyechanjwa ni hatari kwake mwenyewe na wengine, mpeleke akapate chanjo’.

No comments:

Post a Comment