Tuesday, January 15, 2013

Ajali za Barabarani Mkoani Singida zapungua kwa asilimia 12 ikilinganishwa na mwaka juzi.

 Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida Linus Sinzumwa akitoa taarifa yake ya utekelezaji kwa kipindi cha mwaka jana kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha). Kulia ni mwenyekiti mstaafu wa klabu ya waandishi wa habari mchungaji Emmanuel Barnaba na kulia ni diwani wa kata ya Mitunduruni,Pantaleo Sorongai.
 Diwani wa kata ya Utemini manispaa ya Singida Baltazar Kimario akizungumza wakati wa ufunguzi wa tafrija iliyoandaliwa na jeshi la polisi mkoa wa Singida kwa ajili ya kutoa taarifa yake ya utekelezaji kwa kipindi cha mwaka jana na pia kupongeza waandishi wa habari kwa ushirikiano wao mzuri kwa jeshi hilo. Wa pili kutoka kulia ni kamanda wa polisi mkoa wa Singida Linus Sinzumwa.Kutoka kushoto ni mkuu wa magereza mkoa wa Singida na anayefuatia ni diwani wa kata ya Mitunduruni manispaa ya Singida Pantaleo Sorogai.
Baadhi ya waandishi wa habari na maofisa wa jeshi la polisi mkoani Singida waliohudhuria hafla iliyoandaliwa na polisi kwa ajili ya kutoa taarifa yake ya utekelezaji kwa kipindi cha mwaka jana na pia kuwapongeza waandishi wa habari kwa ushirikiano wao mzuri na jeshi hilo.

Jeshi la polisi mkoani Singida kitengo cha usalama barabarani, limekusanya tozo (notification) zaidi ya shilingi 487.9 milioni zilizotokana na makosa mbali mbali ya usalama barabarani kwa kipindi cha mwaka jana.
Akitoa taarifa yake ya utekelezaji ya mwaka jana kwa waandishi wa habari, Kamanda wa polisi mkoa wa Singida Linus Sinsumwa amesema kiasi hicho kilichokusanywa, kimeongezeka kwa asilimia 66.2 ikilinganishwa na kiasi cha shilingi
293,595,000 kilichokusanywa mwaka juzi.
Sinzumwa amesema mafanikio hayo ya kujivunia, yametokana na kitengo cha usalama barabarani kufanya ukaguzi wa mara kwa mara pamoja na kuthibiti makosa ya usalama barabarani.
Katika hatua nyingine, Sinzumwa amesema jumla ya ajali 246 zimetokea  katika kipindi hicho cha mwaka jana ambacho ni sawa na asilimia 20.1 ikilinganisha na ajali 308 za mwaka juzi.
Amesema ajali hizo za mwaka jana zilisababisha watu 139 kupoteza maisha yao sawa na upungufu wa asilimia 12 ya watu 127 waliofariki dunia mwaka juzi kwenye ajali mbali mbali.
Wakati huo huo, kamanda Sinzumwa amesema anaomba uhusiano mkubwa kati ya polisi na waandishi wa habari, uliokuwepo mwaka jana,uendelee hivyo hivyo kwa mwaka huu wa 2013 na uwe wa mafanikio makubwa zaidi.

No comments:

Post a Comment