Monday, January 7, 2013

Taasisi za dini zirudishe tamaduni za kukaa vikao: Rais Kikwete.

 Askofu mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania,(KKKT) Dk.Alex Mwalasusa (aliyesimama) akimsimika askofu mteule wa KKKT dayosisi ya kati Dk.Alex Mkumbo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza kwenye hafla ya kumsimika askofu mteule wa KKKT dayosisi ya kati, Dk.Alex Mkumbo (hayupo pichani).
Rais  Jakaya Kikwete (wa tatu kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Askofu mteule wa KKKT dayosisi ya kati, Dk.Alex Mkumbo na msaidizi wake Cprian Yohana Hilinti (wa pili kulia).Akina mama hao ni wake wa askofu Dk.Mkumbo na msaidizi Hilinti.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.Jakaya Mrisho Kikwete,ameyahimiza madhehebu mbalimbali ya dini nchini, kufufua utaratibu uliokuwepo zamani wa kufanya vikao  baina yao, ambavyo pamoja na mambo mengine,vilisaidia kuimarisha mahusiano mazuri na kuheshimiana.
Dk.Kikwete ametoa wito huo jana (6/1/2013) wakati akizungumza kwenye sherehe za
kusimikwa kwa askofu mteule wa Kanisa la kiinjili la kilutheri dayosisi ya kati,Dk.Alex Seif Mkumbo, kuongoza kanisa hilo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.  Alisema utaratibu huo uliepusha vitendo vya kukashifiana, kudharaulina na kutokuvumiliana.
Alisema hivi sasa vitendo vya kudharauliana,kuchochea vurugu na chuki baina ya madhehebu ya dini,vimechangiwa kwa kiasi kikubwa na kuachwa kwa utaratibu huo ambao ulisaidia mno kudumisha amani na utulivu.
“Hivi sasa watu wanasema sana, wala hawaogopi kusema,mambo sasa hivi ni tofauti mno.Wapo watu wanakipaji cha kuchochea chuki na kuchochea kudharauliana kwa  dhehebu moja na jingine.Bila vikao vya madhdhebu ya dini,watu hawa watasababisha hata uhuru wa kuabudu kutoweka”,alisema na kuongeza; “Utaratibu huu wa kukutana madhehebu kwa madhehebu,utaepusha taifa letu na machafuko  ya kidini”.
Dk.Kikwete alisema kutokana na ukweli huo,upo umuhimu kwa madhehebu ya dini kufufua/kuhuisha utaratibu wa kufanya vikao baina ya madhehebu  ili amani,utulivu,kuheshimiana na kuvumiliana kuweze kudumu.
Aidha,ametumia  fursa hiyo kuwahimiza viongozi wa madhehebu  kutekeleza majukumu yao bila kuchoka ikiwemo kuhimiza uadilifu na kukemea vitendo vyote viovu katika jamii.
Awali askofu mkuu wa KKKT nchni.Dk.Alex Mwalasusa, alimwahidi rais Kikwete kuwa wataendelea kushirikiana na serikali katika kuwaendeleza Watanzania kiroho na kimwili.

No comments:

Post a Comment