Mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Singida,Mgana Msindai (mwenye kofia ya tunga) akikabidhiwa zawadi ya
mbuzi mbili na viongozi wa umoja wa mabasi madogo (Hiace) mjini
Singida.Umoja huo umetoa zawadi hiyo kwa kitendo cha mwenyekiti huyo
kufanikisha mabasi madogo yaanze kutumia kituo cha zamani cha mabasi
mjini Singida.
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Singida Mgana Msindai amewahimiza madereva wa vyombo vya
moto yakiwemo mabasi madogo kutii sheria bila shurti, ili kuepuekana na
usumbufu unaochangia kupoteza muda mwingi.
Msindai
ametoa wito huo wakati akizungumza na viongozi wa umoja wa madereva wa
mabasi madogo (hiece) yanayofanya safari kati ya
Singida mjini na Igunga
mkoani Tabora na Singida mjini hadi Ilongero Singida vijijni.
Amesema
uzoefu unaonyesha wazi kuwa madereva wengi na hasa wa bodaboda na
mabasi makubwa na madogo, huvunja sheria zilizowekwa kwa makusudi lengo
likuwa ni kuwahi abiria.
Msindai
amesema kitendo hicho hupelekea wakamatwe na polisi na kisha kutozwa
faini za papo kwa papo au kufikishwa mahakamani ambapo hupoteza muda
mwingi ambao angeutumia kujiingizia mapato.
Kuhusu
mabasi madogo kuruhusiwa kutumia kituo cha mabasi cha zamani, Msindai
amesema mabasi madogo yameruhusiwa kutumia kituo hicho kwa muda wakati
manispaa ikiendelea kutafuta mwekezaji wa kujenga kitega uchumi.
No comments:
Post a Comment